Jumamosi, 15 Oktoba 2011

WANAWAKE WAWABAKA WANAUME HUKO ZIMBABWE, WAHITAJI MBEGU ZAO KWA USHIRIKINA.



NewsImages/6004758.jpg
Sophie Nhokwara mmoja wa wanawake watatu waliokamatwa kwa kuwabaka wanaume
Uchawi wa mpya umeibuka nchini Zimbabwe ambapo mbegu za uzazi za wanaume zimekuwa dili kiasi cha kundi la wanawake kuwabaka wanaume na kisha kuiba mbegu zao za kiume.
Wanaume kaeni chonjo sasa maana wanawake siku hizi nao wanabaka wanaume kama inavyotokea nchini Zimbwabwe ambapo wanaume wengi wamekuwa wakibakwa au kulazimishwa kufanya mapenzi na wanawake kinguvu ilimradi tu wanawake waweze kupata mbegu zao za kiume.

Kesi za wanaume kubakwa zimeripotiwa kwenye miji ya Gweru, Harare na Mashonaland.

Wanawake watatu wametiwa mbaroni kwenye mji wa Gweru kutokana na matukio ya kuwabaka wanaume waliyoyafanya hivi karibuni.

Wanawake hao watatu walikamatwa kwenye gari lao ambalo walikuwa wakilitumia kama chambo cha kuwavuta wanaume wakijifanya wanawapa lifti.

Ndani ya gari hilo kulikutwa jumla ya kondomu 33 ambazo zilikuwa na mbegu za kiume za wanaume mbalimbali ambao hadi sasa hawajajulikana.

Wanaume wanapokubali kupewa lifti, hutekwa kwa bunduki na kupelekwa sehemu za mbali ambako hulazimishwa kufanya mapenzi na wanawake hao kwa kutumia kondomu au wakati mwingi bila hata kinga huku wakiwa wameelekezewa bunduki. Baada ya hapo wanawake hukusanya mbegu za kiume na kisha huwatupa wanaume waliowateka pembeni ya barabara.

Wanawake waliotiwa mbaroni wametajwa kuwa ni Rosemary Chakwizira mwenye umri wa miaka 24, Sophie Nhokwara mwenye umri wa miaka 26, na Netsai Nhokwara ambaye naye pia ana umri wa 24, wote ni wakazi wa Gweru. Pia dereva wao mwanaume naye ametiwa mbaroni kwa makosa ya kufanya shambulizi nje ya maadili. Dereva huyo pia anatuhumiwa kesi ya mauaji baada ya kumuua kwa kumgonga kwa gari mtoto na kisha kukimbia.

Inasemekana kuwa wanawake hao wamekuwa wakizikusanya mbegu za kiume za wanaume wanaowateka na wamekuwa wakizitumia mbegu hizo za kiume kwenye mambo ya kishirikina.

Wakazi wa Gweru hawakuamini masikio yao pale majina ya wanake hao yalipotajwa kuwa wanabaka wanaume.

"Wanawake hawa wanajulikana sana hapa kwakuwa wamekuwa wakionekana kwenye kumbi za starehe mara kwa mara", alisema mmoja wa wakazi wa Gweru.

Mkazi mwingine wa Gweru aliyejitambulisha kwa jina la Harry Mohammed Misi aliiambia redio moja nchini Zimbabwe "Tumeshtushwa sana na haya yanayotokea kwenye jamii yetu, wanaume sasa nao wanabakwa na wanawake, inaonekana sasa mambo yamebadilika".

Polisi wa Zimbabwe wamesema kuwa watatumia DNA ili kugundua mbegu kiume za wanaume waliobakwa na wanawake hao

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni