Jumapili, 13 Aprili 2014

DARAJA LA MAPINGA BAGAMOYO LIMEBOMOKA KWA MVUA KUBWA INAYOENDELEA KUNYESHA UKANDA WA PWANI.

Wananchi wakiwa hawahamini macho yao wakiangalia sehemu ya daraja la Mapinga Bagamoyo lililokatika kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha ukanda huo, daraja hilo ndilo kiungo muhimu kwa usafiri wa Dar es salaam kwenda Bagamoyo, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, wananchi wameshauriwa kutumia barabara ya Morogoro kwa sasa hadi ukarabati utakapofanyika.

Jumatano, 12 Februari 2014

MAAFISA WAWILI WA TBA WAHUKUMIWA JELA MIAKA TISA KILA MMOJA.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) na mwenzie wamehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela au kulipa faini ya shilingi milioni kumi na tano kila mmoja na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya 2007. Watuhumiwa hao wanadaiwa kwa nyadhifa zao waliidhinisha ujenzi wa jengo la ghorofa 18 katika eneo ambalo mipango miji inaonesha inaruhusiwa kujenga majengo yasiyozidi ghorofa saba tu.

Jumapili, 9 Februari 2014

UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA NAMIKANGO NACHINGWEA WAKUTANISHA VIGOGO WA VYAMA MABALIMBALI. MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA LEO.Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa Bw. Miraji Abdallah pichani katikati.(maktaba)Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Bw. Chikawe yupo naye katika Kampeni.


Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Lipumba juzi alifanya kampeni kumnadi Mgombea Udiwani wake.

Nachingwea, Lindi.
Vigogo wa Vyama mbalimbali vya siasa nchini ikiwemo CCM, CUF,CHADEMA na ADC walimiminika wilayani hapa takribani juma zima lililopita kwa minajiri ya kunadi wagombea wa vyama vyao wa kiti cha Udiwani cha kata ya Namikango, Nachingwea ambacho kipo wazi kwa mwaka mzima sasa baada ya aliyekuwa Diwani wake kufariki mwezi Aprili mwaka jana.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi huo Bw. Kwembe ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, uchaguzi huo utafanyika leo Jumapili tarehe 09/02/2014 kuanzia asubuhi hii hadi saa 10 jioni. Aliongeza kuwa wote watakaokuwa kwenye foleni kufikia muda huo watapiga kura ila watakaofika baada ya muda huo watakuwa wamechelewa, hali ni shwari hadi sasa.
Bw. Miraji Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa ADC aliwasili juzi mjini hapa na jana alifanya mkutano wa kampeni kijijini Namikango, Bw. Freeman Mbowe alitarajiwa juzi na Bw. Chikawe yupo kwa wiki nzima sasa akifanya kampeni za chini kwa chini pia Prof. Lipumba alifanya kampeni na mkutano wa kuimarisha chama hapa mjini Nachingwea. Kwa matokeo ya Uchaguzi wa leo pitia hapa baada ya saa kumi jioni.


Jumapili, 2 Februari 2014

MWENYEKITI WA CCM TAIFA AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO LEO HUKO MBEYA KUADHIMISHA MIAKA 37 YA CCM.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya mshikamano kutoka viwanja vya Soweto Kwenda Bustani ya Jiji jijini Mbeya huku akiwa amewashikilia watoto wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM yanayofanyika leo mkoani Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchema, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula na kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Fedha na Uchumi Mama Zakhia Megji, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi wakishiriki matembezi hayo, Matembezi hayo ya kilomita tano yalianza Saa moja na nusu na kumalizika Saa mbili na robo.
,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kipenzi cha watoto ameshiriki nao katika matembezi hayo kama anavyoonekana akitembea sambamba na watoto hao
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na wana Mbeya mara baada ya kupokea matembezi hayo kwenye bustani ya Jiji jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha Mapinduzi yanayofanyika kwenye uwanja wa Sokoine leo jijini Mbeya.
2A3Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwasili eneo la Soweto 4Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 5Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa kitaifa wa CCMwakiwa wamejipanga tayari kwa kuanza matembezi hayo. 7,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kulia ,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakisonga mbele. 8Maaskari wa vikosi vya usalama Barabarabi na Usalama wa rais wakijiweka sawa na kuupanga msafara wa matembezi hayo 9Wanahabari wakishiriki katika matembezi hayo 10Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kulia akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza barabarani wakati matembezi hayo yakiendelea. 11Adam Gille na wanahabari wengine wakiwajibika kama kawa 12Wananchi wakishiriki katika matembezi hayo 13Mwitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa pamoja na kwamba matembezi hayo yalianza mapema saa moja na nusu mpaka saa mbili na robo.

Jumapili, 26 Januari 2014

MLIPUKO WA GHALA LA SILAHA WAUA ISHIRINI HUKO KONGO DRC


Uharibifu uliotokana na mlipuko

Watu 20 wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko katika ghala la silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo ,vimesema kuwa nyumba nyingi zilaharibiwa wakati wa mlipuko huo katika kambi moja ya kijeshi karibu na soko kuu la Mbuji-mayi.

Kwa mujibu wa taarifa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Monusco,zaidi ya watu 50 pia walijeruhiwa huku nyumba kadhaa zikiharibiwa.Mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mbuji-Mayi inasemekana ulisababishwa na radi
Lengo la Monusco nchini humo ni kupokonya makundi yanayopigana silaha. DRC inajaribu kutokamana na vita vilivyosababisha mamilioni ya vifo kati ya mwaka 1998 na 2003.
'Nimewaamrisha maafisa wetu walio mjini Mbuji-Mayi kushirikiana na wenyeji ili kusaidiana kukabiliana na hali,'' alisema Martin Koble mkuu wa kikosi hicho cha Monusco.
Mbuji-Mayi ni mji wa tatu kwa ukubwa DRC, na ndio kitovu cha uchimbaji wa madini ya Almasi.bbc

Jumamosi, 4 Januari 2014

MAREHEMU MGIMWA KUZIKWA JUMATATU HUKO IRINGA.

Waziri wa Fedha wa Tanzania William Mgimwa, ambaye alifariki siku ya Jumatano kwa sababu za kawaida katika hospitali moja huko Afrika ya Kusini, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu (tarehe 6 Januari), gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti.

Marehemu William Mgimwa.

Mwili wa Mgimwa unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam siku ya Jumamosi, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, William Lukuvi.Mgimwa alifariki katika hospitali ya Mediclinic Kloof ya Pretoria baada ya kulazwa kwa matibabu ya dharura. Mwezi huu angetimia miaka 64.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, Mh. William Lukuvi(Mb)
Siku ya Jumapili, mwili wa Mgimwa utapelekwa Ukumbi wa Karimjee, ambako maafisa na wananchi watatoa heshima zao za mwisho, ikifuatiwa na sala maalumu, Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari.
Mgimwa, mkongwe wa Benki ya Taifa ya Biashara ya Tanzania, alichaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 na kuteuliwa waziri wa fedha mwaka 2012 na ilisifika kwa kuongoza jitihada za Tanzania za kutafuta masoko ya dhamana ya kimataifa ili kugharamia uwekezaji na kukabiliana na umaskini, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP

Jumatatu, 30 Desemba 2013

KAMISHNA ERNEST MANGU ATAAPISHWA KESHO NA RAIS KIKWETE KUWA INSPEKTA JENERALI MPYA BAADA YA IGP MWEMA KUSTAAFU RASMI KESHO.

Kamanda Ernest Mangu ndiye IGP Mteule atakayechukua nafasi inayoachwa wazi na  Inspekta Jenerali Mwema. Anatarajiwa kuapishwa rasmi kesho katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Abdalhman Kaniki ndiye Naibu IGP ikiwa ni cheo kipya katika mfumo wa utawala wa polisi tuliouzoea.