Jumatano, 19 Oktoba 2011

BUSHA LA KILO 45 LAMTESA JAMAA.


NewsImages/6008614.jpg
Wesley Warren Jr
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ana busha lenye uzito wa kilo 45, busha hilo linamtesa sana kiasi cha kushindwa kutembea na hata kwenda chooni.
Wesley Warren Jr anateseka sana kutokana na busha linalomnyima raha na kumfanya ashindwe kuendelea na maisha yake ya kawaida.

Wesley ameanzisha kampuni ya kuchangisha watu pesa ili aweze kupata dola milioni moja ambazo ameambiwa azipeleke hospitali kwaajili ya gharama za operesheni ya kuliondoa busha hilo.

Wesley anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa scrotal elephantiasis. Busha lake ni kubwa sana lenye uzito wa kilo 45 kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea na kupata tabu kwenda haja.

"Ni vigumu sana kutembea, kutwa nashinda ndani", alisema Wesley.

Wesley mwenye umri wa miaka 47, anasema kuwa ingawa baadhi ya watu wanamcheka kutokana na hali yake, hajakata tamaa na aliamua kujitokeza kwenye vipindi vya televisheni na redio kuelezea hali yake ili kuomba msaada wa kuchangisha fedha za operesheni yake.

Hali aliyo nayo Wesley ni nadra sana kuiona kwenye nchi ambazo si za Tropiki zaidi ya Afrika na Asia, ambako ugonjwa huo husababishwa na maambukizi yanayosambazwa na mbu.

Wesley anasema kuwa hajawahi kusafiri kwenye nchi za tropiki na anaamini kuwa hali aliyo nayo inasababishwa na tukio lililotokea mwaka 2008 wakati alipozibana korodani zake katikati ya miguu yake wakati alipokuwa akijigeuza kitandani.

Wesley aliongeza kuwa siku iliyofuatia korodani zake zilivimba na kufikia ukubwa sawa na mpira wa soka

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni