Jumatatu, 24 Oktoba 2011

AGEUKA MWIZI KWA KUPENDA SANA PICHA ZA NGONO



NewsImages/6018254.jpg
Amanda Owens
Mwanamke mmoja wa nchini Marekani amejikuta akigeuka kuwa mwizi na kuwa mashakani kutupwa jela kwa wizi kutokana na tabia yake ya kupenda sana kuangalia video za ngono. Alikuwa akiiba ili apate pesa za kununulia video za ngono.
"Kila mtu na ugonjwa wake" msemo huu unaweza kuwa sahihi kabisa kwa kumaanisha kuwa kila mtu huwa kuna kitu anachokipenda zaidi kuliko vingine.

Amanda Owens mwenye umri wa miaka 18 tu, ugonjwa wake ulikuwa ni kupenda sana kuangalia video za ngono.

Amanda alikuwa akipenda sana kuangalia video za ngono kiasi cha kwamba alikuwa akinunua DVD za video za ngono karibia kila siku.

Pindi alipokuwa hana pesa za kununulia DVD hizo Amanda alikuwa akiiba vitu toka kwa jirani yake na kwenda kuviuza ili apate pesa za kununua DVD hizo.

Amanda mkazi wa St Paul, Minnesota aliajiriwa na jirani yake Darin Pake, 44, kama mlezi wa watoto wake. Lakini mbali ya ulezi, Amanda alianza kumuibia pesa na vitu mbalimbali jirani yake huyo ili aweze kupata pesa za kununua DVD za ngono.

Siku za mwizi zilitimia pale jirani yake huyo alipoamua kuweka kamera za ulinzi ili agundue ni nani aliyekuwa akiiba pesa na mali zake.

Siku mbili tu baada ya kamera hizo za ulinzi kuwekwa, Amanda alinaswa akiiba kamera, brifkesi na kisanduku cha pesa.

Amanda alitiwa mbaroni baada ya jirani yake huyo kuripoti polisi.

Amanda aliwaambia polisi kuwa ndani ya wiki moja alizamia kwenye nyumba ya jirani yake mara tatu na kuiba vitu mbalimbali.

Amanda alitoboa siri polisi kuwa alilazimika kuiba ili aweze kupata pesa za kulipa deni la DVD 30 za ngono ambazo alizinunua hivi karibuni kwa mkopo.

Amanda amefunguliwa mashtaka ya wizi na huenda akatupwa jela miaka 10 pamoja na kutozwa faini ya dola 20,000 iwapo atapatikana na hatia

Maoni 1 :

  1. Unaambiwa maangalizi ya picha hizo ni sawasawa na matumizi ya dawa ya kulevya: mazowea!

    JibuFuta