Jumatatu, 31 Oktoba 2011

OKWI AANGUSHIWA JUMBA BOVU MSIMBAZI, MWAPE ASEMA NI BAO LA MUNGU TU

SIMBA WAWEWESEKA KWA KIPIGO CHA JUZI.

Hivi ndivyo mshambuliaji wa Yanga, Davies Mwape alivyofunga bao pekee dhidi ya Simba. Picha na Jube Tranquilino



Ibrahim Bakari
MUUAJI wa Simba, Davis Mwape amesema ni Mungu tu aliyemwezesha afunge katika mechi yao ya watani iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa juzi ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu.


Mwape alifunga bao pekee katika mchezo huo na kuifanya Yanga kufikisha pointi 24 nyuma ya Simba inayoongoza kwa pointi tatu.


Akizungumza katika mahojiano maalum baada ya mchezo juzi, Mwape alisema: "Ni Mungu kanipa nguvu za ajabu, kufunga katika mechi ngumu ni kazi yake, sikutarajia na wala sikuwa nafikiria kufunga.


"Nasema ni Mungu tu, Mungu amenisaidia sana,


namshukuru na nashukuru pia mashabiki na viongozi wangu na wao kwa kunipa nguvu...," alisema Mwape.


Mwape raia wa Zambia, alisema: "Naamini kile ninachokifanya uwanjani, najua nimecheza vizuri na ndiyo maana nikafunga najitahidi kufanya zaidi ili kufanya maajabu zaidi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni