Jumanne, 4 Oktoba 2011

DK. KAFUMU DALALI NDIYE MBUNGE WA IGUNGA.


NewsImages/5984514.jpg
Dr Dalaly Peter Kafumu baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha ubunge wa Igunga
Mgombea wa CCM wa kiti cha ubunge cha Igunga, Dr Dalaly Peter Kafumu amewagaragaza wagombea wengine saba wa vyama vya upinzani na kushinda ubunge wa jimbo hilo ambalo lilikuwa wazi baada ya kujiuzulu kwa Rostam Aziz.
Katika uchaguzi huo ambao kura zilipigwa siku ya jumapili, Dr Kafumu aliwashinda wagombea wenzake wa jimbo hilo kwa kupata jumla ya kura 26,484.

Mgombea wa CHADEMA, Bw. Joseph Kashindye alishika nafasi ya pili kwa kupata jumla ya kura 23,260 wakati mgombea wa CUF Leopold Mahona alishika nafasi ya tatu kwa kupata jumla ya kura 2,104.

Wagombea wengine watano waliobaki walipata kura chache zisizozidi kura 500.

Jumla ya watu 171,077 walijiandikisha kupiga kura lakini watu wachache sana wapatao 53,672 ndio waliojitokeza siku ya jumapili kupiga kura.

Kwa ushindi huo wa kiti cha ubunge wa Igunga, CCM imeendelea kushikilia viti vyake 259 vya bunge la Tanzania lenye jumla ya wabunge 350.

Chama cha CHADEMA kimebaki na wabunge wake 48 wakati CUF ina wabunge 36

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni