Jumamosi, 8 Oktoba 2011

KIBAKA MSHAMBA WA SIMU ANASWA PICHA YAKE.


Kibaka Aponzwa na Facebook

NewsImages/5992226.jpg
KIbaka aliyetuma picha yake kwenye Facebook
SPolisi wa nchini Marekani wanamtafuta kibaka ambaye alimuibia mtu simu na bila kujijua alijikuta akiituma picha yake kwenye ukurasa wa Facebook wa mmiliki wa simu hiyo.
Polisi wa Georgia nchini Marekani wameanza msako wa kumtafuta kibaka ambaye aliiba simu toka kwenye begi lililoachwa ndani ya gari na bila kujijua alijikuta akijipiga picha ambayo ilikwenda kwenye ukurasa wa Facebook wa mmiliki wa simu hiyo.

Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita wakati mwanamke mmoja mkazi wa McDonough, Georgia alipolipaki gari lake mbele ya shule ya chekechea ili kumchukua mwanae anayesoma kwenye shule hiyo.

Mwanamke huyo alipofika nyumbani kwake aligundua kuwa begi lake ambalo lilikuwa na simu pamoja na vitu vyake vingine lilikuwa limeibwa.

Bahati mbaya kwa kibaka aliyeiba simu hiyo alijipiga picha kwa kutumia simu hiyo na bila kufahamu picha hiyo ilienda moja kwa moja kwenye ukurasa wa mbele wa Facebook wa mmiliki wa simu hiyo.

"Mtuhumiwa alijipiga picha kwa kutumia simu aliyoiiba na kutokana na settings zilizowekwa kwenye simu hiyo, picha hiyo ilienda moja kwa moja kwenye Facebook", alisema afisa wa polisi Jason Bolton.

Afisa huyo wa polisi aliongeza kuwa anaamini kibaka huyo atakuwa anajuta huko aliko kwa kitendo chake cha kujipiga picha.

Picha ya kibaka huyo ilioneka kwenye Facebook siku hiyo hiyo ambayo simu iliibwa na polisi wamefurahi kuwa sura ya kibaka huyo inaonekana wazi wazi.

"Kwa jinsi sura yake inavyoonekana vizuri sana, tuna uhakika hautapita muda mrefu atakuwa ameishatiwa mbaroni", alisema msemaji wa polisi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni