Jumatatu, 3 Oktoba 2011

KILA LA HERI WATAHINIWA MTIHANI KIDATO CHA NNE LEO.




WANAFUNZI wapatao 450,586 wa kidato cha nne leo wameanza kufanya mitihani yao ya kuhitimu elimu hiyo nchini kote
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, alisema kati yao 349,578 ni watahiniwa walio shuleni na 101,105 ni wasio shuleni.

Ndalichako alisema baraza hilo limeandaa mazingira mazuri ya mitihani hiyo na hakuna kuvuja kwa mitihani wala uchakachuaji wa aina yoyote kuhusiana na mitihani hiyo
Wanafunzi wa Sekondari Naipingo Nachingwea, ni kati ya shule zinazofanya mtihani wa kidato cha nne leo, tunawatakia mtihani mwema wanafunzi wote Tanzania wanaoingia kwenye vyumba vya mtihani huo sasa. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni