Jumatatu, 31 Oktoba 2011

NIMEIPENDA HOJA HII, NIMEIKUTA KWA MJENGWABLOG.

Hoja Yangu; Lay Man Ni Nani?

Madaktari wakifanya upasuaji mkubwa. Huwaita wote wasio na taaluma ya udaktari LAY MEN
Wanasheria wakiwa mahakamani. nao huwaita wote wasio wanasheria, LAY MEN
Mapadre na watu wa wakfu.huitwa wenye daraja, na wote wasio na daraja takatifu huitwa LAY MEN.


Wadau nimeshangazwa na madai a makundi haya kwenye jamii.ukitoa maoni kwenye masuala ya kisheria wakati wewe siyo mwanasheria, unaitwa Lay man na wenye fani yao.madaktari nao huwaita wasio madktari kuwa ni lay men, kadhalika na mapadre na watu wenye wakfu huwaita waamini wasio na wakfu lay men.sasa mimi najiuliza, LAY MAN ni nani? na kwa nini hizi profession tatu pekee ndizo zinaita wengine lay men. karibu tujadili
Na Mdau wa Mjengwablog
MAONI YANGU ni kuwa si taaluma hizo tatu tu kuwa huwaita wenzao Lay men, hata ukienda jeshi lolote leo hii eti wanatuita sisi tusio wanajeshi RAIA au Civillian utafikiri wao sio raia wa nchi hii, ukipita Chuo Kikuu kwenye Makongamano yao ndio kabisaa wanajiita WANATAALUMA utafikiri wewe husiye na digrii huna taaluma yoyote, hivyo nakubaliana na mbwembwe zote hizo haina shida, sababu ni kuwa wao ni marafiki wasomi(learned friends) na wamesota kuzipata sifa hizo, hivyo LAY MAN si tusi, ni mtu tu asiye na utaalamu wa kutosha juu ya fani fulani. Naomba kuwasilisha, ni maoni yangu tu Mkuu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni