Jumapili, 29 Mei 2011

SIMBA YATOLEWA KOMBE LA MABINGWA AFRIKA.

Simba Yageuzwa Uchochoro Misri


Sunday, May 29, 2011 2:51 AM
Magoli matatu yaliyofungwa katika dakika tatu za mwisho wa mchezo yameifanya Simba iliage kombe la mabingwa wa Afrika kwa kipigo cha mabao 3-0 toka kwa timu ya Wydad Casablanca ya Morocco.
Klabu ya Simba imeshindwa kuwika mbele ya timu ya Wydad Casablanca ya Morocco baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mechi ya kombe la mabingwa wa Afrika iliyochezwa kwenye uwanja wa Petrosport Stadium jijini Cairo nchini Misri.

Magoli matatu yaliyoiua Simba yalifungwa ndani ya dakika tatu za mwisho wa mchezo huo ambao kipa wa Simba, Juma Kaseja alifanya kazi ya ziada kuiokoa michomo mikali ya washambuliaji wa Wydad Casablanca.

Goli la kwanza la Wydad Casablanca lilifungwa kwenye dakika ya 87 na Allou Mustapha ambaye dakika moja baadae aliifungia timu hiyo goli la pili. Wydad Casablanca waliongeza goli la tatu kwenye dakika za majeruhi.

Kwa kipigo hicho, Simba imetolewa kwenye kombe la mabingwa wa Afrika na sasa itarudi kucheza kwenye kombe la shirikisho la CAF kwa kuanzia mechi za raundi ya tatu ambapo itapimana ubavu na timu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kongo.

CHANZO; Nifahamishe.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni