Jumamosi, 14 Mei 2011

AMCHINJA MTU NA KUKIMBIA NA KICHWA CHAKE.

Amchinja Mtu na Kukimbia na Kichwa Chake MtaaniSaturday, May 14, 2011 11:51 AM
Watalii katika mji wa Tenerife nchini Hispania hawakuamini macho yao pale mwanaume mmoja alipojitokeza ghafla na kumshambulia mwanamke raia wa Uingereza na kukikata kichwa chake na kuanza kutimua mbio mitaani akiwa amekishikilia mkononi kichwa hicho.

Mwanaume huyo anayeaminika kuwa ni raia wa Bulgaria ambaye alikuwa hana makazi maalumu akilala mitaani katika mji wa Tenerife, alimvamia mwanamke raia wa Uingereza na kumshambulia kwa panga hadi alipokinyofoa kichwa chake na kisha kutimua mbio mitaani akiwa amekibeba kichwa hicho.

Watalii hawakuamini macho yao kwa tukio hilo ambalo lilifananishwa na matukio ya kwenye sinema.
Mwanaume huyo alifanya mauaji hayo ndani ya supermarket baada ya kuiba panga toka kwenye duka la vitu vya kitamaduni la Wachina.

Mwanaume huyo mwenye rekodi ya uhalifu alimvamia mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50, na kuanza kumshambulia kwa panga akijaribu kukikata kichwa chake kama anachinja kuku hadi alipofanikiwa.

Akizishikilia nywele kwenye kichwa cha mwanamke huyo, alianza kutimua mbio akikiacha kiwiliwili huku damu zikiendelea kuchuruzika kwa wingi.

Walinzi wa supermarket walianza kumkimbiza mwanaume huyo ambaye aliangushwa chini alipotandikwa na helmet ya mwendesha pikipiki alipokatiza mbele yake akiwa amekibeba kichwa hicho.

"Nilipaki gari langu na ghafla nilimuona mwanaume akitoka kwenye supermarket akiwa ameshikilia kitu chenye kuchuruzika damu kwenye mikono yake huku walinzi wakimkimbiza" alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo.

"Alikitupa kitu hicho pembeni ya barabara, kiliangukia pembeni yangu nilipoangulia vizuri niligundua kilikuwa ni kichwa cha mwanamke", aliendelea kusema shuhuda huyo.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa mwanaume huyo raia wa Bulgaria alikuwa akijulikana sana maeneo hayo na alikuwa hamjui mwanamke huyo aliyemchinja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni