Jumatano, 4 Mei 2011

BWAWANI HOTELI YAKODISHWA KWA BEI POA.



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Hoteli yake ya Bwawani itapoteza jumla ya shs 228,000,000 ( Millioni Mia Mbili na Ishirini na Nane) kwa mwaka kwa maamuzi yake ya kukodisha ukumbi wa disco wa hoteli hiyo kwa kampuni ambayo imetowa tenda ndogo.

Kampuni iliyopewa tenda ya kukodishwa ukumbi huo ni ya National Marketing Company ambayo ni Kampuni tanzu ya Chama cha Mapinduzi iliyouundwa mwaka 1999.

Taarifa zinasema kuwa Serikali ilitangaza tenda ya ukodishwaji wa ukumbi huo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana na kampuni tatu zilijitokeza kutaka biashara hiyo.

Ukumbi huo ulikuwa chini ya National Marketing tokea mwaka 2004 ambapo iliupata kwa njia zisizokuwa za tenda na uendeshaji wake umekuwa ukisimamiwa na Hussein Ibrahim Makungu wa DJ Bhaa Style.

Habari zimeeleza kuwa Kampuni ya Star Times ilitoa ofa ya kutaka kukodishwa kwa shs 34,000,000 (Millioni 34) kwa mwezi, Zenj FM ikawa taayri kulipa shs 24,000,000 ( Millioni 24) kwa mwezi na National Marketing wao wakawa tayari kuweka mezani shs 15,000,000 kwa mwezi.

Katika hatua isioeleweka mantiki yake Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo imetoa tenda hiyo kwa National Marketing ha hivyo moja kwa moja kuchukua tenda ndogo na kuiweka serikali katika naasi ya kukosa mapato makubwa zaidi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Abdillahi Hassan Jihad hadi sasa amekataa kusaini upewaji wa baishara hiyo kwa kampuni ya National Marketing kwa madai ya kukosa maelezo ya kutosha kuhusu uamuzi huo.

Inaaminika kuwa Hussein Ibrahim Makungu ameshailipa Nationa Marketing t shs 60,000,000 lwa kodi ya awali ya miezi 4, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa fedha ambazo zimeingia Bwawani kutoka National Marketing ni t shs 40,000,000.

Haikuweza kueleweka mara moja ni kwa nini National Marketing haikuwasilisha kiasi kizima hicho kwa Hoteli ya Bwawani.

Mbali ya kwamba Serikali imeingia katika mkataba wa hasara, habari za ndani ya Hoteli hiyo zinasema kuwa kama Hoteli hiyo itaweza kusimamia wenyewe mradi huo kikamilifu ikiwa ni ukumbi wa disco na eneo la bwawa la kuogelea, hoteli inaweza kuingiza karibu ya shs 700,000,000 (Millioni Mia Saba) kwa mwaka.

Juhudi za hoteli hiyo kutaka kuapta uendeshaji wa asilimia 100 zilifanyika huko nyuma pale Hoteli ilipoweza kununua vifaa vya muziki vyenye thamani ya dola za kimarekani 50,225.

Lakini vifaa hivyo vikachukuliwa na kusambazwa kwa hla na katika taasisi zilizofaidika na hilo ni pamoja na bendi ya Big Star na vikundi vyengine huko Pemba. Deni la ulipaji wa vyombo likawaganda Hoteli ya Bwawani.

Katika Mkataba uliotiwa saini Agosti 12, 2005 kuna kipengele kinachosema kuwa Mkodishwaji atalipa vifza hivyo, lakini hakuna rekodi zinazoonyesha kuwa deni hilo limelipwa na Bhaa Style.

Ukodiswaji wa ukumbi na bwawa la hoteli hiyo umekuwa wa mipango mipango kw muda mrefu. Awali ulikodishwa kwa Chuchu Sounds kwa mgawano wa asilimia 35 kwa Chuchu Sounds na 65 kwa Bwawani. Kisha ikapewa timu ya Miembeni kwa mgawano wa asilimia 40 kwa Miembeni na Bwawani asilimia 60.

Novemba 2004 National Marketing ilianza kuwa na mkataba wa wazi na Hoteli ya Bwawani ambapo Bwawani ikiwakilishwa na Andrew Katema ilipata asilimia 65 na National Marketing ikiwakilishwa na Haji Omar Kheri ilipata asilimia 35.

Agosti 11, 2005 mkataba mwengine ulitiwa saini baina ya pande hizo mbili na huu ulikuwa ni miwezi minne ukiisha Disemba 2005 lakini kwa masharti dhalili zaidi dhidi ya Serikali kupitia Hoteli ya Bwawani.

Badala ya Mgawano wa 65-35 mkataba huu mpya ulisema Mkodishwaji alipe kiasi cha shs 1,500,000 ( mIllioni Moja na Nusu) kwa kila mwezi kwa jumla ya shs 18,000,00 kwa mwaka mmoja. Hili kwa hakika Mkodishaji alilitimiza kikamilifu.

Wadau ndani ya Hoteli ya Bwawani wanasema hilo limetimizwa maana ni fedha ndogo sana kutakiwa alipe Mkodishaji kwa jinsi biashara hiyo ambayo sasa ni ya kila siku inavyoingiza na hili limeonekana baada ya kutangazwa tenda ambapo kiwango cha chini kilichopendekezwa kulipwa nishs 15,000,000 na cha juu ni shs 34,000,000 kwa mwezi.

Taarifa zinasema mradi huo wa disco uliendelea kushikiliwa na National Marketing kupitia Bhaa Style bila ya mkataba wowote kuanzia Januari 2006 hadi Disemba 2010.

Imeelezwa kuwa uamuzi wa kuikodisha National Marketing kwa bei ya chini na kuacha tenda zenye fedha nyingi zaidi umezua msugauno sio tu ndani ya Wizara lakini pia ndani ya Hoteli hiyokwa vile kitendo hicho kinainyima Hoteli ya Bwawani fedha zaidi na hivyo kujiendesha wenyewe.

Wafanyakazi wa Hoteli ya Bwawani wametaka Serikali iliingilie kati suala hilo ili kuiepusha Serikali na hasara inayoweza kuepukika wakisema mambo kama hayo ndio yanayofanya ionekane kuwa hoteli hiyo ni mzigo na wala haiwezi kabisa kujisimamia seuze kujiendesha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni