Jumamosi, 7 Mei 2011

NANI MKALI WA TASNIA YA VICHEKESHO NCHINI? KUJULIKANA LEO USIKU MANGO GARDEN KINONDONI.

King Majuto

Joti

Masele

Masanja

Kingwendu

Fainali ya mkali wa vichekesho itafanyika leo usiku katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni ukiwashirikisha magwiji wa vichekesho waliofanikiwa kuingia tano bora wakiwemo King Majuto, Kingwendu, Joti, Masele na Masanja Mkandamizaji.

Mshindi wa kwanza anatarajiwa kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi za kitanzania milioni moja na nusu, wa pili milioni moja , wa tatu laki tano na wanne na tano laki mbili na nusu kila mmoja. Burudani za vikundi mbalimbali vya muziki itakuwepo kusindikiza onesho hilo.

Wadhamini ni pamoja na Allure International Model,Dsm City College, Girraffe Hotel, Jarida la Malaika, Cream Pub-Kinondoni, Dotnata Decoraton, Manywele Beauty Cosmetics na ASSET Ltd.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni