Alhamisi, 19 Mei 2011

ANOLD AZAA NA YAYA WAKE.


Anold na aliyekuwa yaya wake.

Ndoa ya miaka 25 ya mcheza filamu maarufu duniani na gavana wa jimbo la California, Arnold Schwarzenegger imevunjika na sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo imeelezwa kuwa ni baada ya Arnold kumla uroda na kumzalisha hausigeli wake.
Ndoa ya Arnold Schwarzenegger ambayo ilivunjika wiki iliyopita imeelezwa kuwa kitendo cha Arnold Schwarzenegger kuwa na uhusiano wa kimapenzi na hausigeli wake ndio chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo.
Majarida ya udaku ya Marekani yalifanya uchunguzi wa kina kumgundua kimada wa Schwarzenegger baada ya Schwarzenegger mwenye umri wa miaka 63, kumuomba msamaha mkewe wake Maria Shriver na familia yake akisema kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa yao ni mtoto wa nje ya ndoa ambaye alizaa na hausigeli wake miaka 10 iliyopita.
Hausigeli huyo ametajwa kuwa ni Mildred Patricia Baena na kwa miaka 20 alikuwa akifanya kazi za ndani nyumbani kwa Arnold kama vile kupika, kufua nguo, kuosha vyombo na kazi nyingine za ndani na alikuwa akipokea mshahara mzuri wa dola 1,200 kwa wiki.
Patricia ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 50 amestaafu kazi za ndani na anaishi kwenye nyumba yake kubwa ya vyumba vinne yenye bwawa la kuogelea pamoja na mtoto huyo wa Arnold ambaye sasa ana umri wa miaka 10. Patria ana watoto wengine watatu aliozaa na mwanaume mwingine.
Jarida la udaku la TMZ lilisema kuwa Arnold alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Patricia kwenye miaka ya 1990 na Patricia aliwahi kuwaambia marafiki zake kuwa alikuwa akifanya mapenzi na Arnold bila ya kutumia kinga ndani ya nyumba ya Arnold.
Alipopata ujauzito hakumwambia Arnold ambaye baadae alikuja kugundua baada ya mtoto huyo wa kiume kuzaliwa.
Kufuatia kugundulika kwa siri hizo za ndani, mke wa Arnold, Maria Shriver mwenye umri wa miaka 55, ametangaza kuwa atatoboa siri zote atakapoenda kwenye shoo ya Oprah Winfrey baadae mwaka huu.
Shriver na Arnold wana watoto wanne ambao ni Katherine, 21, Christina, 19, Patrick, 17, na Christopher mwenye umri wa miaka 13

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni