Alhamisi, 12 Mei 2011

FOMU YA UENYEKITI UVCCM SHILINGI LAKI MOJA TU.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umetangaza na kuwataka vijana wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa Taifa katika umoja huo.

Mh. Masauni, Mwenyekiti aliyejiuzulu.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Mfaume Kizigo, alitangaza hayo jana wakati alippokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Kutangazwa na nafasi hiyo kumekuja baada ya kumtafuta mrithi wa aliyekuwa Mwenyekiti ngazi hiyo, Hamad Masauni kujiuzulu kwa mujibu wa kanuni za UVCCM, Ibara ya 95.

Kizigo alisema fomu kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo zitaanza kutolewa leo kwa gharama ya shilingi. 100,000 na mwisho ya kuchukua fomu ni Mei 20, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kizigo, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ilitoa maelekezo na ratiba ya uchaguzi huo ambapo Juni Mosi hadi 30 vikao vya mchujo ambavyo ni Sekretarieti, Kamati ya Utekelezaji na Baraza Kuu la UVCCM vitakaa na kuanzia Julai Mosi hadi 30 kutakuwa na vikao vya uteuzi vya CCM.

Alisema mgombea pia anapaswa kuwa mwanachama hai wa UVCCM na CCM anayetimiza haki, wajibu na masharti ya uachachama na awe raia wa Tanzania

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni