Jumapili, 29 Mei 2011

GESTI ILIYOKUWA INASUMBUA WANAFUNZI YAFUNGWA NA UONGOZI WA SERIKALI KATA YA KIGOGO.

The Queens Gest yafungwa


Kufungwa kwa nyumba hiyo kumekuja baada aya gizo kutoka kwa Meya na makubaliano yaliyofanyika baina ya uongozi huo na mmiliki wa gesti hiyo.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kigogo, Emmanuel Riwa alibainisha kuwa, katika mazungumzo hayo walikubaliana nyumba hiyo mmiliki huyo aibadilishe kutoka ya kulala wageni na iwe katika mfumo wa kawaida ya kupangisha watu kwa ajili ya makazi

Alisema nyumba hiyo kwa muda uliobaki utapangisha kama makazi kusubiria shughuli ya tathimini na ulipaji wa fidia itakapokamilika kutoka Manispaa kwa ajili ya mazingira hayo kuwa ya shule.

Hata hivyo pia wameadhimia kufunga gesti hiyo kutokana na kuona inachangia mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi wa sekondari hiyo .

Wanafunzi washule hiyo walioongea na nifahamishe walionekana kufurahishwa na hatua iliyochukulia na Meya wa Kinondoni na kusema nyumba hiyo ingeweza kuwaporomosha kimasomo kutokana usomaji ulikuwa mgumu

“Yaani tumefurahi ujue nyumba yenyewe ilikuwa ikitoza shilingi 1,500 kiwango cha chini, ingeweza kuharibu wanafunzi wanaopenda ngono za utotoni kwa kuwa wangekuwa na uwezo wa kulipia”walisema

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni