Alhamisi, 26 Mei 2011

HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE TOKA IRINGA ZINASEMA MAJAMBAZI YATEKA MAGARI MLIMA KITONGA USIKU WA JANA KUAMKIA LEO.


Magari yakipanda mlima Kitonga.

Majambazi hayo yalifunga barabara hiyo kuanzia saa 8 usiku hadi pale polisi toka kituo cha Ilula walipofika na kuwasambaratisha, baadhi ya madereva wanasema walilazimika kurudi nyuma hadi Kitonga Comfort Hotel wakisubiri kupambazuke ili wapite. Habari kuhusu majeruhi bado hazijathibitishwa toka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni