Alhamisi, 5 Mei 2011

MKE WA WAZIRI AFRIKA YA KUSINI AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Sheryl Cwele, mke wa waziri A kusini

Bi Sheryl Cwele
Sheryl Cwele, mke wa waziri wa masuala ya kijasusi, amekutwa na hatia ya kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Cwele, aliyeolewa na Siyabonga Cwele, alikuwa akiajiri wanawake kuingiza dawa hizo nchini Afrika kusini kutoka Uturuki na Marekani ya kusini.

Madai ya biashara ya dawa za kulevya yalianza mwaka 2009 baada ya kukamatwa kwa mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini aliyekamatwa Brazil na aina ya cocaine yenye thamani ya dola za kimarekani 300,000.

Tessa Beetge kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka nane gerezani mjini Sao Paulo.

Alikutwa na kilo 10 za coaccaine kwenye mkoba wake.

Cwele alikutwa na hatia pamoja na mwenzake Frank Nabolisa, raia wa Nigera, katika mahakama kuu ya Pietermaritzburg.

Watu hao wawili, ambao walikana mashtaka, wanakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela. Hukumu inatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa.

Upinzani umetoa wito wa kumtaka Bw Cwele ajiuzulu, ukisema kama hajui shughuli za mkewe zilizo kinyume cha sheria, basi hana haja ya kuendelea kuongoza kitengo cha kijasusi nchini humo.

Mwandishi wa BBC Milton Nkosi aliripoti kutoka Johannesburg kwamba Bw Cwele hakuwepo mahakamni siku ya Alhamis na hajasema lolote kuhusu kutiwa hatiani kwa mkewe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni