Jumapili, 15 Mei 2011

PAKISTAN YAILAUMU MAREKANI

Pakistan: Marekani inatuharibia jina
Bunge la Pakistan limeitaka serikali izingatie tena uhusiano wa nchi hiyo na Marekani, baada ya Osama bin Laden kuuliwa na kikosi cha Marekani.

Bunge limedai ndege za Marekani zisokuwa na rubani ziache kufanya mashambulio katika ardhi ya Pakistani, na lilisema inafaa kufikiria kuacha kuruhusu vifaa vya NATO vinavokwenda Afghanistan, kupitia Pakistan.

Wabunge piya walitaka uchunguzi ufanywe kuhusu operesheni ya kumuuwa Osama bin Laden, ambayo waliilaani kuwa imevunja mamkala ya Pakistan.

Maazimio yaliyopitishwa na bunge hayakutaja swala la vipi kiongozi wa Al Qaeda alifika kuwa nchini humo. Badala yake, kikao hicho cha faragha cha bunge kilijadili uhusiano maalum baina ya Pakistan na Marekani.

Maazimio yamelaani sana shughuli za Marekani nchini humo, na kile kilichoelezewa kuwa "kampeni ya Marekani kuipa Pakistan jina baya".

Bunge halikuilaumu idara ya usalama ya Pakistani hadharani.

Wabunge waliohudhuria kikao hicho cha faragha, walisema, mkuu wa Idara ya Ujasusi, Jenerali Pasha, alichagizwa sana na baadhi ya wabunge, na alisema yuko tayari kujiuzulu; ingawa Waziri Mkuu hajakubali ombi la jenerali huyo .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni