Jumamosi, 21 Mei 2011

MWANAMIELEKA WA WWE AFARIKI DUNIA.



Gwiji wa mieleka ya Kimarekani Randy Savage au maarufu kwa jina la Macho Man
Saturday, May 21, 2011 12:02 AM
Gwiji wa mieleka wa Marekani, Randy Savage au maarufu kwa jina la Macho Man amefariki dunia kutokana na ajali ya gari.
Gwiji wa mieleka ya Kimarekani Randy Savage au maarufu kwa jina la Macho Man ameiaga dunia asubuhi ya leo kwa saa za marekani, (Majira ya saa 11 jioni kwa saa za TZ) baada ya kupata ajali ya gari karibu na nyumba yake iliyopo kwenye kitongoji cha Seminole, Florida.

Macho Man amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58 na alikuwa maarufu sana duniani kutokana na umahiri wake kwenye mieleka kuanzia kwenye miaka ya 1980.

Macho Man alipata ajali baada ya kushindwa kuukontroo usukani wa gari lake la mwaka 2009 modeli ya Jeep Wrangler alilokuwa akiliendesha.

Taarifa zilisema kuwa gari lake lilivuka zege linalotenganisha barabara na kwenda upande wa pili wa barabara ambapo lilisimama baada ya kuugonga mti uliopo pembeni ya barabara.

Alifariki kwenye hospitali ya jirani kutokana na majeraha aliyopata, taarifa ya polisi imethibitisha kuwa Macho Man hakuwa akiliendesha gari hilo huku amelewa.

Macho Man katika anga ya mieleka aliwahi kuwa bingwa wa WWE mara mbili, bingwa wa dunia wa uzito wa juu kwenye mieleka mara mbili na pia alikuwa bingwa wa mabara kwa miezi 14.

Taarifa kamili juu ya sababu ya kifo chake itatolewa baada ya uchunguzi wa maiti yake kukamilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni