Jumamosi, 21 Mei 2011

SHEIKH YAHYA KUZIKWA LEO SAA SABA MCHANA MAKABURI YA TAMBAZA MUHIMBILI.

Wasifu mfupi wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein
21/05/20110 Comments Mdogo wa marehemu Sheikh Yahya Hussein bwana Abdallah Juma amesema kuwa kaka yake:

Alizaliwa miaka 89 iliyopita katika mtaa wa Mkunguni Kipande, Kariakoo, Dar es Salaam.

Kabila lake likiwa ni Mmanyema, mwenyeji wa Kigoma.

Alisoma shule ya kati ya Uhuru, Dar es Salaam kabla ya kuhamishiwa Zanzibar kwa Sheikh Abdallah Saleh Farqy, alikojifunza Kurani na baadae kwenda nchini Misri na kujiunga na Chuo cha Al Adhar cha Cairo.

Alikuwa mwalimu wa Kurani, kwa kuisoma na kuifundisha.

Alianza kuupata umaarufu tangu alipokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Waislamu wa Afrika Mashariki katika miaka ya 1950.

Alianza masuala ya unajimu na utabiri wa nyota mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Kuhusu kifo chake, mtoto wa marehemu aitwaye, Hussein Yahya, alisema baba yake:

Alifariki dunia jana saa tano asubuhi, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda wa miaka miwili.

Alifariki dunia akiwa katika Hospitali ya Mount Ukombozi, Kinondoni ambapo alipelekwa jana asubuhi kwa matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya.

Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Sala ya kumwombea marehemu imepangwa kufanyika katika Msikiti wa Tambaza majira saa nne adhuhuri.

Maziko yake yatafanyika leo saa saba mchana katika makaburi ya Tambaza.

Ameacha mjane, watoto 15 na wajukuu kadhaa.

Hadi alipofariki jana alikuwa na ofisi mjini London, Uingereza, Nairobi, Kenya, Botswana, Swaziland na Tanzania, za kazi zake alizokuwa akifanya enzi za uhai wake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni