Alhamisi, 19 Mei 2011

RAIA WA GHANA AMUHOFIA STRAUSS-KAHN

Bw Strauss-Khan
Wakili wa mfanyakazi aliyemshutumu mkuu wa shirika la fedha la kimataifa (IMF) Dominique Strauss-Kahn kwa udhalilishaji amesema "anaogopa" lakini atatoa ushahidi dhidi yake.
Jeffrey Shapiro amesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32 aligundua kuwa aliyemdhalilisha ni Bw Strauss-Kahn siku moja baada ya tukio hilo na kumfanya ahofie maisha yake pamoja na ya binti yake.
Alisema " kulikuwa hakuna makubaliano yoyote kwa kilichotokea katika chumba hicho cha hoteli" mjini New York Mei 14.
Bw Strauss-Kahn amekana mashtaka yote.
Mwanamke huyo ameiambia polisi ya New York kwamba Bw Strauss-Kahn alijaribu kumbaka na alimtambua katika zoezi maalum la utambulisho.
Anashtakiwa kwa vitendo vya uhalifu vinavyohusiana na ngono, jaribio la kumbaka, udhalilishaji wa kijinsia, kumfungia kinyume cha sheria na kumshika bila ridhaa yake.
Bw Straus-Khan, mwenye umri wa miaka 62, anaangaliwa kwa makini kwa kuhofia kujiua katika gereza la kisiwa cha Rikers mjini New York.
Atarejea mahakamani siku ya Ijumaa.
Mke wake, aliyekuwa mtangazaji wa televisheni ya Ufaransa Anne Sinclair, anadhaniwa kwenda kumtembelea siku ya Jumatano.
Wakati huo huo, waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner alisema Bw Staruss-Kahn hastahili kuwa mkuu wa shirika hilo la fedha na jina mbadala litajwe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni