Mtoto Fatma Hassan katikati akiwa na wenzie mara baada ya kumaliza swala ya Eid msikiti wa Majengo J leo asubuhi huko Nachingwea.
Amani yabidi idumishwe miongoni mwa wanadamu ili watoto kama hawa wakue katika maadili mema na wafurahie maisha.
KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com
> | ||
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema hatua hiyo imekuja kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia. Alisema kuwa bei hiyo ni kutokana na mabadiliko ya bei ya bidhaa za mafuta katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na Dola ya Marekani. Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei ya mafuta zitaendelea kupangwa na soko na kukokotolewa kila baada ya wiki mbili Hivyo aliwataka wafanyabiashara na wateja wakubaliane na bei hizo zitakazopangwa na Ewura kwa kuwa bidhaa za mafuta zinabadilika mara kwa mara na kuomba kuepukana na migomo isiyo na tija. Masebu amevitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei ya bidhaa hiyo katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei halali iliyotolewa na mamlaka hiyo na wanu uzi kudai stakabadhi halali na tarehe aliyonunulia mafuta Mkoa wa Dar es Salaam sasa Petrol itakuwa kwa Sh2,070, dizeli ni Sh1,999 na mafuta ya taa Sh1,980. Bei kikomo Kikanda mikoani inaonyesha kuwa bei ya petroli kwa Mkoa wa Arusha sasa ni Sh 2,154, dizeli ni Sh2,083 na mafuta ya taa Sh2,064. Mkoa wa Dodoma petroli itauzwa kwa Sh2,128, dizeli Sh2,058 na mafuta ya taa Sh2,038. Mwanza petroli sasa ni Sh2,219, dizeli Sh2,149 na mafuta ya taa Sh2,130. Mkoa wa Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,176 , dizeli Sh2,106 na mafuta ya taa kwa Sh2,087. Mkoa wa Kigoma petroli itauzwa kwa Sh2,301, dizeli Sh2,230 na mafuta ya taa Sh2,211 |
Teams | P | GD | PTS | |
---|---|---|---|---|
1 | Liverpool | 3 | 4 | 7 |
2 | Chelsea | 3 | 3 | 7 |
3 | Wolves | 3 | 3 | 7 |
4 | Man City | 2 | 5 | 6 |
5 | Man Utd | 2 | 4 | 6 |
6 | Aston Villa | 3 | 2 | 5 |
7 | Wigan | 3 | 2 | 5 |
8 | Newcastle | 2 | 1 | 4 |
9 | Bolton | 3 | 1 | 3 |
10 | Everton | 2 | 0 | 3 |
11 | QPR | 3 | -5 | 3 |
12 | Stoke City | 2 | 0 | 2 |
13 | Sunderland | 3 | -1 | 2 |
14 | Norwich | 3 | -2 | 2 |
15 | Swansea | 3 | -4 | 2 |
16 | Arsenal | 2 | -2 | 1 |
17 | Fulham | 2 | -2 | 1 |
18 | West Brom | 2 | -2 | 0 |
19 | Tottenham | 1 | -3 | 0 |
20 | Blackburn | 3 | -4 | 0 |
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Kabwe Zitto aliyesimama wakati akitoa hoja hiyo Bugneni jana | JANA Bunge lililazimika kusitisha shughuli zake za kawaida ili na kuingiza majadiliano dhidi ya Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo kuhusiana na kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo | |
Hayo yamekuja baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini [Chadema], Kabwe Zitto kuwasilisha hoja ya kuliomba Bunge liahiishe shughuli zake na kujadili maamuzi hayo Uamuzi uliotolewa na Luhajnjo uligusa hisia za wabunge walio wengi na kuushangaza Umma kutokana na maamuzi hayo kuonekana kuingilia na kudharau Bunge akiwemo na kudhalilishwa kwa Waziri Mkuu “Naliomba Bunge lisitishe kujadili hoja zote za Serikali hadi hapo ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali hadi hapo ripoti ya iliyomsafisha Jairo itakapofikishwa Bungeni” alisema Zitto Zitto aliwasha moto huo majira saa 3:18 asubuhi mara baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kufungua bunge hilo “Mheshimiwa Naibu Spika unafahamu ya kwamba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizungumza ndani ya Bunge hili ya kwamba angekuwa ni yeye angeshamchukulia hatua Ndugu Jairo kuhusu vitendo alivyofanya, hivyo basi naomba nitoe hoja kwamba Bunge lisitishe hoja yoyote ya Serikali mpaka itakapoleta bungeni taarifa ya CAG kuhusiana na uchunguzi huo.” Baada ya kutoa hoja hiyo, Zitto aliungwa mkono na wabunge zaidi ya nusu waliokuwamo ndani ya ukumbi huo na kusikika miungurumo ya makofi, hali ambayo ilimlazimisha Naibu Spika wa Bunge, Ndugai, kuitisha Kamati ya Uongozi kwa dharura kujadili suala hilo. Baada ya kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya Bunge, Ndugai alirejea ukumbini na kutoa taarifa kuwa kikao hicho kiliongozwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda na kukubaliana na hoja ya Zitto kwa kupima hoja iliyotolewa kuwa ni nzito hivyo tunaunda Kamati teule kuhusiana na sakata hilo Mara baada ya kutoa tangazo hilo wabunge walifurahia majibu hayo na kuzizima kwa shangwe kufurahia kuundwa kwa kamati teule |
Jairo hana hatia, atakiwa kuanza kazi mara moja | ||
Davidi Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini | Wednesday, August 24, 2011 10:59 AMKATIBU Mkuu Kiongozi Bw. Phillemon Luhanjo ameamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo aliyesimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi dhidi yake aanze na kurejea kazini mara moja kwa kuwa uchunguzi umebaini hana hatia | |
Jairo, alisimamishwa kazi Julai 21, mwaka huu, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa bungeni wakati wa kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo ambapo alidaiwa kuchangisha jumla ya shilingi. bilioni moja kuwahonga wabunge ili waweze kupitishe bajeti ya wizara hiyo. Luhanjo alisema uchunguzi huo ulikuwa chini ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG] Ludovick Otouh na kubaionika Jairo hana hatia yoyote Imefafanuliwa kuwa, katika mapitio ya uchunguzi huo ulipitia nyaraka mbalimbali, vitabu vya risiti, hati za malipo na taarifa za benki kwa kipindi cha mwezi Mei hadi Julai mwaka huu Uchunguzi huo umebaini taasisi zipatazo nne zilichanga kiasi cha shilingi milioni 149.7. zilichangwa kupitia taasisi hizo na si 20 kama ilivyodaiwa awali na si kiasi cha shilingi bilioni moja kilichoaiwa na baadhi ya wabunge Ukaguzi huo pia haukupata ushahidi wowote wa fedha zilizochangwa kutumika kuwalipa wabunge malipo yoyote kwa madhumuni ya kuwahonga bali malipo yaliyofanyika yalihusu posho za kujikimu, takrima na posho za vikao kwa maofisa walioshiriki katika kazi nzima ya uwasilishwaji wa bajeti hiyo. Hatua ya kusimamishwa kwa Bw. Jairo ilikuja baada ya tuhuma zilizotolewa na wabunge wakati wa bajeti ya awali ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo walidai kuwa Bw. Jairo amechangisha jumla ya shilingi. bilioni moja kutoka kwenye taasisi 20 zilizo chini ya wizara hiyo kwa lengo la kuwahonga wabunge kupitisha bajeti hiyo |
Tariq Aziz | Monday, August 22, 2011 4:37 AMAliyekuwa naibu waziri mkuu wa Iraq enzi za utawala wa rais Saddam Hussein, Tariq Aziz ameitaka serikali ya Iraq imnyonge mapema iwezekanavyo kwa kuwa amechoka kusubiri huku akiteseka kwa magonjwa mbali mbali. | |
Tariq Aziz, alikuwa naibu waziri mkuu wa Iraq enzi za utawala wa Saddam Hussein na alihukumiwa kunyongwa kama bosi wake mwezi oktoba mwaka jana. Rais wa Iraq, Jalal Talabani alikataa kutia sahihi adhabu ya kunyongwa kwa Tariq Aziz badala yake alitaka hukumu hiyo hiyo iwe kifungo cha maisha. Baada ya kutupwa jela akisubiri suluhisho la hukumu yake, Tariq Aziz amemtaka waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki afanye mipango ya haraka ili anyongwe kwasababu amechoka kusubiri huku akiteseka kwa magonjwa yanayomkabili. "Afya yake ni mbaya sana, ameniomba nimwambie Maliki awahishe kunyongwa kwake mapema iwezekanavyo", alisema mwanasheria wa Tariq Aziz, Badie Aref. "Amesema hili ndio ombi lake kwa sasa kwa kuzingatia afya yake anateseka", alisema Aref. Aref aliongeza kuwa Tariq Aziz amekuwa akihudumiwa vizuri sana jela lakini amekuwa akisumbuliwa na magonjwa ya kisukari, presha, vidonda vya tumbo na kansa. Tariq alihukumiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mauaji na kuvunja haki za binadamu. Saddam Hussein ambaye naye alipatikana na hatia ya makosa kama hayo alihukumiwa kunyongwa na alinyongwa disemba 30 mwaka 2006 ambayo ilikuwa ni siku ya kwanza ya sikuu ya Idi |