Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SOKA-BBC. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SOKA-BBC. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 23 Agosti 2011

NASRI HUENDA AKATUA MANCHESTER CITY KWA PAUNI MILIONI 25 MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

Nasri katika mechi ya jumamosi na Liver.

Nasri leo asubuhi alifanya mazoezi na Arsenal, sasa yupo njiani kuelekea mjini Manchester.

Manchester City wamekubaliana na Arsenal kumsajili kiungo Samir Nasri. Nasri sasa anaelekea mjini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya.
Nasri alifanya mazoezi na Arsenal siku ya Jumanne asubuhi kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Udinese, utakaochezwa Jumatano. Hata hivyo jina lake liliondolewa kwenye orodha ya wachezaji.
Kiungo huyo kutoka Ufaransa anakwenda Manchester pia kukamilisha mkataba wake ambao unadhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25.
Meneja wa City, Roberto Mancini alisema siku ya Jumapili kuwa anataka kumsajili Nasri ndani ya kipindi cha saa 48.

Jumatatu, 15 Agosti 2011

CESC FABREGAS ATUA BARCELONA RASMI

Cesc Fabregas tayari ni mchezaji rasmi wa Barcelona baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ulaya.
Cesc Fabregas
Cesc Fabregas


Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal amefuzu uchunguzi wa afya yake aliofanyiwa mara mbili siku ya Jumatatu na atatambulishwa na klabu hiyo wakati wowote.
Arsenal itapokea kitita cha paundi milioni 30 na paundi milioni 5 nyingine zitatolewa kutegemeana na idadi ya mechi atakazocheza na vikombe itakavyoshinda Barcelona.
Siku ya Jumapili, Arsenal na Barca walithibitisha "kukubaliana kimsingi" juu ya kumuuza Fabregas.
"Tunaelewa hamu aliyonayo Cesc ya kurejea katika klabu ya nyumbani kwao na sasa ameafikiana na klabu ya Barcelona," alisema meneja wa Arsenal, Arsene Wenger.
"Tumekuwa tukifahamisha bayana hatukutaka Cesc aondoke na hali hiyo inasalia hivyo hivyo.
"Tunamshukuru Cesc kwa mchango wake katika klabu ya Arsenal na tunamuombea mafanikio huko aendako."
Barcelona imekuwa ikimuwinda Fabregas tangu msimu uliopita.
Cesc Fabregas
Cesc Fabregas

Taarifa za mpango wa kuuzwa kwa Fabregas zilithibitishwa wakati wa kipindi cha mapumziko kwenye mchezo wa awali wa kuwania Kombe la Hispania siku ya Jumapili, ambapo Barcelona ilitoka sare ya mabao 2-2 na Real Madrid.
Fabregas tayari ameshafanyia uchunguzi wa awali wa afya yake katika hospitali iitwayo Hospital de Barcelona.
Fabregas alifanya mazungumzo na wachezaji wenzake wa Arsenal kwa mara ya mwisho siku ya Ijumaa asubuhi na hakuwemo katika kikosi cha Wenger kilichocheza siku ya Jumamosi dhidi ya Newcastle katika mechi ya ufunguzi wa msimu ambapo timu hizo hazikufungana.
Hakuwemo katika ziara ya timu ya Arsenal barani Asia na pia hakucheza mechi nyingine za kujiandaa kwa msimu mpya wa ligi, zikiwemo mechi za Kombe la Emirates, kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya msuli wa paja.
Fabregas
Fabregas

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania, ameshaichezea nchi yake mechi 58 na kwa klabu ya Arsenal amecheza mechi 303 wakati wa kipindi cha miaka minane akiwa kaskazini mwa jiji la London na amefunga mabao 57 katika mashindano yote aliyocheza.
Mwezi wa Oktoba mwaka 2003, alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo kuichezea Arsenal katika kikosi cha kwanza, ambapo mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Rotherham United kuwania kufuzu kwa Kombe la Carling wakati huo akiwa na umri wa miaka 16 na siku 177.
Pia alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo wa klabu hiyo kufunga bao, alipofunga wakati Arsenal ilipilaza Wolves mabao 5-1 mwezi wa Desemba mwaka huo wa 2003. Fabregas alikuwa katika kikosi cha Arsenal kilichoilaza Manchester United kwa mikwaju ya penalti na kushinda Kombe la FA mwaka 2005, na kuwa kombe muhimu la pekee aliloshinda na Arsenal kwa muda wote akichezea klabu hiyo.
Aliteuliwa kuwa nahodha wa Arsenal mwezi wa Novemba mwaka 2008. Mshambuliaji Robin van Persie anatazamiwa kuchukua nafasi ya unahodha wa kudumu wa Arsenal, ingawa hatacheza mechi dhidi ya Udinese baada ya kufungiwa kutokana na kadi nyekundu aliyooneshwa msimu uliopita walipocheza na Barcelona katika moja ya mechi za Ubingwa wa Ulaya.
Alipobanwa kuhusiana na mustakabali wa Fabregas na Samir Nasri - BBC ikifahamu fika naye yupo njiani kuelekea Manchester City -kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Wenger alisema anatumai "hakuna yeyote atakayeihama" Arsenal

GERVINHO AZUA BALAA LIGI UINGEREZA.

Joey Barton kiungo wa Newcastle amekiri "alianguka kirahisi" wakati wa purukushani na Gervinho lakini akasisitiza mshambuliaji huyo wa Arsenal alistahili kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Joey Barton

Joey Barton

Gervinho alitolewa katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya England akiichezea Arsenal kwa kumchapa kibao Barton, ambaye naye alioneshwa kadi ya njano kwa kumsukasuka Gervinho.
Baada ya kwenda sare ya 0-0, Barton aliandika katika mtandao wa tweeter: "Nilijiangusha kirahisi sana, hakuna ubishi kwa hilo. Lakini bado huwezi kuinua mikono yako. Mwamuzi alitenda haki, hakukosea."
"Iwapo unainua mikono yako na kumpiga mwenzio usoni, huna budi kutolewa nje. Watu walitaka nifanyeje, nisimame na kuanza kurusha ngumi?"
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alisema wachezaji wote wawili walipaswa kupewa adhabu inayofanana.
Siielewi ile kadi nyekundu," alisema Wenger. "Nina hakika asilimia 100 mwamuzi hakuona kilichotokea.
"Nadhani alikuwa amegeuka upande mwengine wakati purukushani zikitokea. Iwapo aneona tukio lenyewe, angewatoa nje wachezaji wote wawili au asingemtoa yeyote."
Wachezaji hao walishikana baada ya Gervinho kuanguka chini eneo la sanduku la timu ya Newcastle na Barton akamfuata kwa hasira na kuanza kumkunja fulana ya Gervinho.



"Kwa nini Joey Barton alikwenda pale na kuanza kumkunja fulana yake na kumuinua?" aliongeza Wenger. "Ni kadi ya manjano kwa wote au kadi nyekundu kwa wote na kilichotokea hakikuwa kikubwa sana.
Kuhusu kukata rufaa? Nitaangalia tukio lile kwa makini kwanza, lakini nadhani ninashawishika kusema nitakata rufaa."
Meneja wa Newcastle Alan Pardew alimtetea Barton, ambaye yupo katika orodha ya wachezaji wanaohama katika klabu hiyo baada ya kuishutumu klabu na alipangwa mechi ya Jumamosi baada ya kumshawishi meneja wake kwamba hana nia ya kuhama tena.
"Gervinho alijiangusha, hakuna tatizo na hilo," alisema Pardew. "Jinsi alivyofanya Joey kumfuata ilikuwa ni kumtia adabu na kukatokea kutoelewana. Lakini baadae akamchapa kibao na huwezi kufanya hivyo."

Alhamisi, 4 Agosti 2011

NYOTA WA SOKA WA JAPAN AFARIKI DUNIA.

Mcheza kandanda wa Japan Naoki Matsuda amefariki dunia siku mbili baada ya kupoteza fahamu uwanjani akiwa mazoezini ikidhaniwa ni matatizo ya moyo.
Naoki Matsuda
Naoki Matsuda


Matsuda aliyekuwa na umri wa miaka 34, aliyeiwakilisha Japan katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002, siku ya Jumanne alikimbizwa.
Alianguka na kuzimia akifanya mazoezi na klabu yake ya Matsumoto Yamaga, na tangu wakati huo hakuweza kurejewa na fahamu.
Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya Japan, Philippe Troussier akitoa rambirambi zake kwa familia ya mchezaji huyo, alisema alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha nchi hiyo kilichoshiriki Kombe la Dunia.
"Inasikitisha sana kuona mtu anafariki dunia akiwa na umri mdogo kama wake," Bw Troussier alieleza Shirika la Reuters.
"Ni pigo kubwa. Alikuwa kijana mzuri sana na nilikuwa karibu naye. Niko pamoja na jamaa zake katika msiba huu mkubwa."
Mashabiki, marafiki na wachezaji wenzake wa zamani, walikusanyika katika hospitali ya Matsumoto kumtakia apone haraka alipokuwa amepoteza fahamu.
Matsuda aliichezea Japan mara 40 na kushinda mataji mara mbili katika Ligi ya nchi hiyo katika kipindi cha miaka 15 cha uchezaji wake na timu ya Yokohama F-Marinos.
Mapema mwaka huu alijiunga na timu ya Matsumoto inayocheza ligi ya chini

Jumatatu, 25 Julai 2011

BALOTELLI AANZA TENA VITUKO UWANJANI, MANCINI AMTOA NJE.


Mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika mechi yao dhidi ya LA Galaxy kwa kutoonyesha heshima kwa wapinzani wake.
Mancini na Balotelli

Mshambulizi huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 20 alikuwa karibu kufunga goli,lakini hakufunga na badala yake akapiga mpira kwa kisigino na kukosa kufunga.
Kocha wa Manchester City Roberto Mancini alimpumzisha Balotelli kutokana na tukio hilo lakini wakati akitoka nje ya uwanja akajibizana na kocha wake.
Awali Balotelli alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti katika mechi hio ya kirafiki ilomalizika kwa sare ya 1-1.
Man City Imepata ushindi wake wa tatu katika mechi zake za kujiandaa kwa msimu wa ligi kuu ya England.Katika uwanja huo mashabiki wa LA Galaxy walimzomea Balotteli kwa kitendo chake hicho.
Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Inter kujikuta katika matatizo na Kocha Mancini, ambaye pia alikuwa kocha wake nchini Italia

Ijumaa, 8 Julai 2011

LIVERPOOL KUMSAJILI CHARLIE ADAM TOKA BLACKPOOL.

 

Mchezaji Charlie Adam

Liverpool imekubaliana na Blackpool kuhusu kuhama kwa mchezaji Charlie Adam.
Adam, mwenye umri wa miaka 25, amewasili kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na kujadiliana kuhusu masuala yake binafsi.

Mwezi Januari alikuwa karibu ajiunge na Tottenham lakini muda wa kuhama kwa wachezaji ukamalizika kabla ya wao kuafikiana kuhusu kandarasi yoyote.
Iwapo Adam atajiunga na Liverpool, atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na meneja Kenny Dalglish tangu walipomaliza katika nafasi ya sita kwenye ligi kuu ya England msimu uliopita.

Mchezaji mwengine, Jordan Henderson, alijiunga na Liverpool kutoka Sunderland mwezi Juni kwa kiasi cha pauni za Uingereza milioni £20m.
Golikipa wa Roma Alexander Doni pia huenda akajiunga na Liverpool katika saa 36 zijazo, haya ni kwa mujibu wa wakala wake Ovidio Colucci.
Timu zote zilikubaliana kuhusu kuhama kwa Doni mwezi uliopita lakini walikuwa hawajakubaliana kuhusu masharti yake binafsi.

Jumapili, 12 Juni 2011

MICHUANO YA CAF AFRIKA; SIMBA SC YAICHAPA MOTEMA PEMBE BAO 1-0

Shirikisho linaloongoza mchezo wa mpira wa miguu CAF linasema kuwa Libya bado ndiyo iliyopangiwa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013.
Hata hivyo Caf linasema kuwa mipango mbadala ipo ikiwa Libya itashindwa kutokana na ghasia za sasa hivi nchini humo.
Waasi wanaotaka kumpindua Kanali Mummar Gaddafi wanadhibiti sehemu kubwa ya mashariki ya nchi hiyo.
Katibu mkuu wa CAF Hicham El Amrani ameiambia BBC kuwa mashindano yote ambayo Libya ilikubali kuandaa siyo tu Kombe la Mataifa ya Afrika bali hata mashindano ya wachezaji wanaocheza soka katika vilabu vya nyumbani CHAN na Futsal bado tunaonelea kuwa ni jukumu la Libya.
Libya iliahidi kuandaa
Mipango mingine ipo

Katika kinyanganyioro cha vilabu klabu ya JS Kabylie imekuwa ya kwanza kufuzu kwa hatua za makundi katika Kombe la shirikisho kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya ASC Jaraaf ya Senegal mechi iliyochezwa ijumaa mjini Tizi Ouzou.
J.S KABYLIE
Mshambuliaji wa Kabylie

Mabao ya Kabylie yalitiwa kimyani na beki Chemseddine Nessakh na kiungo Saad Tedjar kutimiza jumla ya mabao 3-1 kwa klabu hiyo ya Algeria.
Ikumbukwe kuwa klabu hiyo JS Kabylie ilikuwa bingwa wa Afrika mwaka 1981 na 1990.
Wakati huo huo Kufuatia ushindi wa Asec Mimosas ya Ivory Coast wa 4-0 dhidi ya Primeiro Agosto ya Angola katika mchuano wa kwanza na kutoka sare ya 1 1 katika mecghi ya marudiano nchini Angola, Asec Mimosa inapiga hatua kwa ushindi wa jumla ya bao 5-1 il hali Primeiro itabidi isubiri msimu ujao.
Wakati Primeiro ya Angola ikisubiri fursa ya kushiriki michuano ya Afrika mwakani, watani wao Inter Clube ilisababisha sare ya 2-2 ugenini Morocco dhidi ya klabu ya nchini humo Difaa al Jadida, mechi ya kwanza mjini Luanda ilimalizika kwa Difaa kudundwa matatu kwa bwerere.
Entente Setif ya Algeria ilikuwa nchini Nigeria kuchuana na Kaduna united baada ya ushindi wa 1-0 nchini Algeria tunasubiri matokeo ya mchuano wa mjini Kaduna leo.
mgogoro nchioni Libya
CAF inatafakari mwenyeji mwingine

Na mgogoro wa Libya umeanza kuathiri ratiba ambapo mechi kati ya Sunshine stars ya NIGERIA na Al Ittihad ya Libya ilibadilishwa ifanyike kwa mkondo mmoja badala yua miwili ikitazamiwa kuchezwa kati ya tareh 10 na 12 juni yaani leo
Huko Fez nchini Morocco,l Zesco united ya Zambia ilikuwa uwanjani kwa matumaini ya kuongezea ushindi wao wa bao moja kwa sufuri majuma mawili mjini Lusaka lakini waligutushwa kwa bao mbili za Maghreb Fez na hivyo Fez inapiga hatua kwa ushindi wa 2-1.
Mjini Dar es Salaam Tanzania Simba ya Dar es Salaam illipokea klabu ijulikanayo kama Darling Club Motema Pembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Simba Sports au mnyama kama wapenzi wake wanavyopenda kumuita alimtafuna Motema Pembe 1-0 bao lililotiwa kimiani na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi.
Licha ya ushindi huo Simba ina kibarua itakapochuana na Motema Pembe katika mechi ya marudiano mjini Kinshasa jumapili ijayo. Ina maana Simba haitoweza kupumzika.
Kwa upande mwingine mjini Nairobi Sofapaka iliwapa matumaini mashabiki wake licha ya kuingia uwanjani ikiwa na deni la bao 3-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Club Africain majuma mawili yaliyopita.
Sofapaka ilitumia vizuri uwanja wa nyumbani na kuisukuma Club Africain na kupata magoli matatu ingawa Africain iliweza kufunga bao moja la ugenini.
Bao hilo la ugenini la Africain ndiyo lililoiondoa Sofapaka na kuhitimisha safari yake.

Alhamisi, 2 Juni 2011

SEPP BLATTER ACHAGULIWA TENA FIFA.

Sepp Blatter na Afrika

Sepp Blatter ameteuliwa tena bila ya kupingwa kwa kipindi kingine cha miaka minne kuwa Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA.
Sepp
Sepp Blatter mara tu baada ya kuchaguliwa tena

Kuteuliwa kwa Bw Blatter kunafanyika huku kukiwa na mgogoro mkubwa ndani ya shirikisho hilo kuhusu madai ya rushwa katika mchakato wa kuwania nafasi za kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.
Je, Sepp Blatter anagusa vipi soka barani Afrika? Mwandishi wetu Mohammed Allie ameandika tathmini ifuatayo kutoka Cape Town, Afrika Kusini.
Jibu la swali hili, litategemea unaongea na nani.
Nchini Afrika Kusini, Sepp Blatter anachukuliwa kuwa ama ni shujaa au ni muovu.

Ukakamavu

Wapenzi wengi wa soka wa Afrika ya Kusini wanaamini kwamba ni kutokana tu na juhudi na ukakamavu wa Rais wa FIFA ndio hatimae bara la Afrika lilipata fursa ya kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka uliopita; ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 80 ya michuano hiyo, na kwa ajili hiyo daima watamshukuru raia huyo wa Uswisi mwenye umri wa miaka 75.
Baada ya juhudi za Afrika Kusini kuandaa michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2006 kushindwa katika hali ya utata mkubwa, Blatter aliazimia kuhakikisha kuwa kombe la dunia linakwenda Afrika kwa kuanzisha mfumo wa kupokezana kati ya mabara ya dunia ambapo nchi tano za Afrika zilichuana kuwania nafasi ya kutayarisha michuano ya 2010 .

Heshima

Serikali ya Afrika ya Kusini ilimtunukia Blatter heshima kuu ya Oliver Tambo kwa mchango wake wa kupeleka michuano ya kombe la dunia nchini humo.
Wengine wanaamini Blatter aliiburuza kamati ya matayarisho pamoja na serikali kujenga viwanja vipya na miundo mbinu iliyohusika na kombe la dunia vilivyogharimu fedha nyingi bila ya lazima wakati nchi ilikuwa na mahitaji mengine muhimu katika nyanja ya afya, umeme, maji na usafi.

Dikteta

Wanatoa mifano ya viwanja ambavyo havitumiki sana nchini humo kama urithi wa fedha ziliopotezwa. Wakosoaji wake pia wanamuona Blatter kuwa ni mtu mjanja na dikteta ambae aliidhibiti vilivyo Afrika ya Kusini katika kipindi kabla na wakati wa michuano ya kombe la dunia.

Hata hivyo si siri kwamba Afrika imenufaika sana wakati wa enzi ya miaka 13 ya Blatter kama Rais wa FIFA.
Ilikuwa chini ya uongozi wake kwamba uwakilishi wa Afrika katika michuano ya Kombe la Dunia uliongezeka kufikia mataifa matano na baadae kiwango cha rikodi cha mataifa sita katika michuano ya mwaka 2010 baada ya kujumuisha mwenyeji Afrika Kusini.

Mafunzo

Wakati wa utawala wake FIFA imewekeza takriban dola nusu billioni barani Afrika kupitia huduma, vituo vya mafunzo, mkiwemo viwanja vinavyoweza kutumika majira yote pamoja na mipango ya kutoa mafunzo kwa waandishi habari na maafisa wa utawala.
Kwa mfano kituo cha maendeleo cha Rwanda, kimezaa matunda yake ya kwanza kwa timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 17 kufaulu kushiriki katika michuano ya kombe la dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 17 yatakayoanza nchini Mexico baadae mwezi huu.
Mchukie mpende, Fifa chini ya Sepp Blatter imetoa mchango mkubwa kwa bara la Afrika ambao umepindukia mipaka ya kandanda.

Jumatano, 25 Mei 2011

BIRMINGHAM YAFUTA ZIARA YA TANZANIA.

City
Birmingham City

Birmingham City wameamua kufuta safari yao ya kwenda Tanzania.
City, ambao wameshuka daraja katika ligi kuu ya England msimu huu walikuwa wasafiri kwenda Tanzania kupambana na Simba ya Yanga katika mechi za kirafiki.
Hata hivyo watayarishaji walishindwa kuthibitisha utaratibu wa safari hiyo katika muda waliopewa.
Mabingwa hao wa kombe la Carling sasa wanatafuta nchi ya kwenda kucheza mechi za za kabla ya kuanza kwa msimu.

Jumatano, 27 Aprili 2011

MAN U YAICHAPA SCHALKE MABAO MAWILI.

Manchester United imepiga hatua kubwa kuelekea katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kuifunga Schalke katika nusu fainali ya kwanza nchini Ujerumani.
Giggs
Giggs amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga goli katika michuano hii

United wangeweza kufunga mabao mengi kabla ya mapumziko, kama sio uhodari wa kipa wa Schalke, Manuel Neuer.
Hata hivyo United walipata bao la kwanza katika kipindi cha pili, baada ya Wayne Rooney kupenyeza pasi wa Ryan Giggs. Rooney baadaye alipachika bao la pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Javier Hernandez.
United itaikaribisha Schalke kwenye uwanja wa Old Trafford, Jumatano tarehe 4 mwezi Mei, kwa ajili ya mchezo wa pili wa nusu fainali.
Iwapo watadhibiti ushindi wao, United itawakilisha soka ya England katika Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley.

Jumatano, 20 Aprili 2011

MAN-U YAKABWA KOO

Manchester yabanwa na Newcastle

Manchester United imebanwa na Newcastle kwenye uwanja wa St James Park na hivyo kutoa matumaini kwa Arsenal na Chelsea katika kuwania ubingwa.
Newcastle
Newcastle

United inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 70 ikiwa imesalia michezo mitano.
Javier Hernandez na Wayne Rooney walikosa nafasi nzuri walipobaki na kipa, lakini Ryan Giggs alikosa bao kwa kupiga mkwaju wake nje.
Stephen Ireland angeweza kuipatia ushindi Newcastle, lakini mkwaju wake pia ulitoka nje.