Ijumaa, 26 Agosti 2011

BUNGE LAMUUNDIA KAMATI JAILO


NewsImages/5908358.jpg
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Kabwe Zitto aliyesimama wakati akitoa hoja hiyo Bugneni jana
JANA Bunge lililazimika kusitisha shughuli zake za kawaida ili na kuingiza majadiliano dhidi ya Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo kuhusiana na kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo
Hayo yamekuja baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini [Chadema], Kabwe Zitto kuwasilisha hoja ya kuliomba Bunge liahiishe shughuli zake na kujadili maamuzi hayo

Uamuzi uliotolewa na Luhajnjo uligusa hisia za wabunge walio wengi na kuushangaza Umma kutokana na maamuzi hayo kuonekana kuingilia na kudharau Bunge akiwemo na kudhalilishwa kwa Waziri Mkuu

“Naliomba Bunge lisitishe kujadili hoja zote za Serikali hadi hapo ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali hadi hapo ripoti ya iliyomsafisha Jairo itakapofikishwa Bungeni” alisema Zitto

Zitto aliwasha moto huo majira saa 3:18 asubuhi mara baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kufungua bunge hilo

“Mheshimiwa Naibu Spika unafahamu ya kwamba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizungumza ndani ya Bunge hili ya kwamba angekuwa ni yeye angeshamchukulia hatua Ndugu Jairo kuhusu vitendo alivyofanya, hivyo basi naomba nitoe hoja kwamba Bunge lisitishe hoja yoyote ya Serikali mpaka itakapoleta bungeni taarifa ya CAG kuhusiana na uchunguzi huo.”

Baada ya kutoa hoja hiyo, Zitto aliungwa mkono na wabunge zaidi ya nusu waliokuwamo ndani ya ukumbi huo na kusikika miungurumo ya makofi, hali ambayo ilimlazimisha Naibu Spika wa Bunge, Ndugai, kuitisha Kamati ya Uongozi kwa dharura kujadili suala hilo.

Baada ya kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya Bunge, Ndugai alirejea ukumbini na kutoa taarifa kuwa kikao hicho kiliongozwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda na kukubaliana na hoja ya Zitto kwa kupima hoja iliyotolewa kuwa ni nzito hivyo tunaunda Kamati teule kuhusiana na sakata hilo

Mara baada ya kutoa tangazo hilo wabunge walifurahia majibu hayo na kuzizima kwa shangwe kufurahia kuundwa kwa kamati teule

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni