Jumatatu, 15 Agosti 2011

EWURA YASALIMU AMRI KWA WAFANYABIASHARA.


EWURA Yasalimu Amri, Yapandisha Bei ya Mafuta

NewsImages/5881366.jpg
Godwin Samwel, Meneja Biashara Ewura alipokuwa akitoa taarifa mbele ya vyombo vya habari jana
Monday, August 15, 2011 3:52 PMBAADA ya kumalizika kwa mgomo ambao umetingisha jiji na mikoa tofauti hapa nchini kwa ajili ya kupunguzwa kwa bei,jana Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeongeza tena bei ya mafuta inayoanzwa kutumika leo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Biashara Ewura,Bw. Godwin Samwel alisema wamepandisha bei ya mafuta kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania katika soko la dunia

Bei hizo zimebainishwa kuwa petroli imepanda na kufikia Sh. 100.34 , dizeli Sh. 120.47 na mafuta ya taa kwa Sh 100.87 hizo ni bei kwa lita moja

Amesema kuwa bei hizo mpya zinaonyesha bei ya nishati hiyo katika soko la dunia kupanda kwa wastani wa asilimia 5.42, huku thamani ya shilingi ya Tanzania ikiwa imeshuka kwa Sh 47.12 sawa na asilimia 2.96 kwa dola moja ya Marekani.

Mbali na kutoa bei hiyo mpya pia aliwaagiza wauzaji wa mafuta nchini kuuza bei elekezi na isizidi bei hiyo kwani wanaweza kuuza bidhaa za mafuta kwa bei ya ushindani alimradi bei hizo zisivuke kikomo.

Wakati huohuo mkoani Dodoma Wilayani Mpwapwa imeripotiwa kuwa siku ya tatu leo hakuna mafuta katika vituo vitoavyo huduma hiyo kwa madai ya kutokuwepo kwa mafuta hayo.

Chanzo: www.nifahamishe.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni