Jumatano, 24 Agosti 2011

KATIBU MKUU JAIRO AREJEA OFISINI LEO.


Jairo hana hatia, atakiwa kuanza kazi mara moja

NewsImages/5905466.jpg
Davidi Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
Wednesday, August 24, 2011 10:59 AMKATIBU Mkuu Kiongozi Bw. Phillemon Luhanjo ameamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo aliyesimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi dhidi yake aanze na kurejea kazini
mara moja kwa kuwa uchunguzi umebaini hana hatia
Jairo, alisimamishwa kazi Julai 21, mwaka huu, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa bungeni wakati wa kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo ambapo alidaiwa kuchangisha jumla ya shilingi. bilioni moja kuwahonga wabunge ili waweze kupitishe bajeti ya wizara hiyo.

Luhanjo alisema uchunguzi huo ulikuwa chini ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG] Ludovick Otouh na kubaionika Jairo hana hatia yoyote

Imefafanuliwa kuwa, katika mapitio ya uchunguzi huo ulipitia nyaraka mbalimbali, vitabu vya risiti, hati
za malipo na taarifa za benki kwa kipindi cha mwezi Mei hadi Julai mwaka huu

Uchunguzi huo umebaini taasisi zipatazo nne zilichanga kiasi cha shilingi milioni 149.7. zilichangwa kupitia taasisi hizo na si 20 kama ilivyodaiwa awali na si kiasi cha shilingi bilioni moja kilichoaiwa na baadhi ya wabunge


Ukaguzi huo pia haukupata ushahidi wowote wa fedha zilizochangwa kutumika kuwalipa wabunge malipo yoyote kwa madhumuni ya kuwahonga bali malipo yaliyofanyika yalihusu posho za kujikimu, takrima na posho za vikao kwa maofisa walioshiriki katika kazi nzima ya uwasilishwaji wa bajeti hiyo.

Hatua ya kusimamishwa kwa Bw. Jairo ilikuja baada ya tuhuma zilizotolewa na wabunge wakati wa bajeti ya awali ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo walidai kuwa Bw. Jairo amechangisha jumla ya shilingi. bilioni moja kutoka kwenye taasisi 20 zilizo chini ya wizara hiyo kwa lengo la kuwahonga wabunge kupitisha bajeti hiyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni