Ijumaa, 12 Agosti 2011

HATI YA MASHTAKA YA WAKILI MAARUFU YAREKEBISHWA, POLISI BADO WAENDELEA KUMSHIKILIA.

Wakili Median Mwalle

Peter Saramba, Arusha
UPANDE wa mashtaka tayari imefanyia marekebisho na kuwasilisha mahakamani hati ya mashtaka dhidi ya wakili maarufu nchini, Mediam Mwale, anayekabiliwa na madai ya kujihusisha na uingizaji zaidi ya Sh18 bilioni nchini kinyume cha taratibu.Hati hiyo ilirejeshwa na kupokelewa kwenye masjala ya mahakama juzi, lakini haikuweza kusomwa mbele ya hakimu kutokana na mshtakiwa kutofikishwa mahakamani baada ya kulazwa hospitalini.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Charles Magesa, Agosti 9, mwaka huu alikataa kupokea hati ya awali iliyokuwa na mashtaka 13 iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Velitas Mlau, kutokana na kujaa makosa ya kisheria.

Miongoni mwa makosa ya kisheria yaliyotajwa na Wakili wa utetezi, Loomu Ojare, ni hati hiyo kutotaja wazi wazi jina la kampuni, taasisi, shirika wala mtu aliyetoa au kumpa mshtakiwa fedha zinazodaiwa kuingizwa nchini kinyume cha sheria.

Wakati huohuo, habari za uhakika zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, zinasema wakili huyo alipelekwa hospitali baada ya kulalamika kujisikia vibaya.

“Ingawa sijajua kwa usahihi nini tatizo linalomkabili hadi niwasiliane na mamlaka husika hospitali ya serikali alipolazwa, lakini ni kweli tulimpeleka Mount Meru baada ya kusema anajisikia vibaya,” alisema Andengenye.

Andengenye lisema hadi jana alikuwa hajapata taarifa iwapo wakili huyo bado yupo hospitali au ameruhusiwa na kuahidi kufuatilia.
Juhudi za kupata taarifa rasmi za tatizo linalomsumbua Mwale kutoka kwa madaktari wa Hospitali ya Mount Meru, zilikwama baada ya wahusika kugoma kulizungumzia, huku akitupa suala hilo kwa polisi.

“Kweli tumempokea na kumpa huduma ya afya mtu huyo unayemtaja. Lakini siwezi kuzungumzia zaidi suala hilo kwa sababu liko mikononi mwa polisi. Pia, siwezi kueleza tatizo linalomkabili kwa sababu ni kinyume cha taratibu na sheria za kitabibu kutaja siri ya mgonjwa, labda kama yeye atakuwa tayari kusema,” alisema mmoja wa madaktari kwa sharti la kutotajwa.


Polisi aliyekuwa zamu kumlinda Wakili Mwale hospitalini hapo aligoma kumruhusu mwandishi wa habari hizi, kumwona au kuzungumza naye huku akisisitiza lazima kipatikane kibali kutoka kwa Kamanda wa Polisi Wilaya (OCD) au mkoa (RPC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni