Jumanne, 2 Agosti 2011

MWANAUME AKUTWA NA VIA VYA UZAZI VYA KIKE.



Mkulima mmoja wa nchini India ambaye pia ni baba wa watoto wawili amewashangaza madakatri baada ya kugundulika mbali ya kuwa ni mwanaume rijali tumboni mwake ana viungo vyote vya kike vya kumuwezesha mwanamke kupata ujauzito.
Mkulima huyo aliyetambulika kwa jina la Ryalu aliwahishwa hospitali baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo.

Wakati madaktari wakimfanyia upasuaji wakidhani anasumbuliwa na ugonjwa wa kidole cha tumbo, walipigwa na butwaa walipogunudua mwanaume huyo ana mfumo kamili wa uzazi wa kike.

Tumboni mwake mbali ya kwamba kulikuwa na mfumo kamili wa uzazi wa kiume pia kuligundulika kuna mfumo kamili wa uzazi wa kike kukiwa na mji wa mimba, mayai ya uzazi ya kike, nyonga, mirija ya fallopian na tishu za sehemu ya siri ya kike.

Madaktari wa hospitali katika mji wa Bhopal, Madhya Pradesh, walishangazwa kugundua viungo hivyo vya uzazi vya kike vikiwa kwenye sehemu ya chini ya tumbo la Ryalu.

Daktari Pramod Kumar Shrivastava, wa hospitali hiyo alisema kwamba Ryalu kwa nje hana tofauti na wanaume wengine, alikuwa na viungo vyote vya uzazi vya kiume na alikuwa akiishi maisha ya kawaida kama mkulima.

"Tumeviondoa viungo vyote vya uzazi vya kike na hivi sasa anaendelea vizuri", alisema daktari Shrivastava.

Taarifa zaidi ziliongeza kwamba Ryalu hakuwahi kusumbuliwa na matatizo yoyote ya tumbo hadi hivi karibuni alipokumbwa na maumivu makali tumboni na kuwahishwa hospitali.

"Hana matatizo yoyote ya kijinsia, homoni zake zote ni za kiume na hana matiti kwenye kifua chake", aliongeza dakati mwingine wa hospitali hiyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni