Alhamisi, 18 Agosti 2011

MSICHANA AFIA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO UPENDO MJINI MTWARA.

Mtwara Mnarani, kielelezo muhimu kuwa umeingia Manispaa ya Mtwara-Mikindani

Msichana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Rose na inasemekana ni mwanachuo wa chuo cha Utumishi wa umma hapa mjini Mtwara amekutwa amekufa asubuhi ya jana katika Gesti iitwayo Upendo maeneo ya Ligula Kiyangu mjini Mtwara. Kijana mmoja ambaye ni dereva wa taxi maeneo ya Bima aitwaye Bakari ndiye aliyetoa taarifa ya tukio hilo kituo kikuu cha polisi Mtwara akieleza kuwa alikuwa na msichana huyo usiku wote na kugundua kuwa huenda kafa nyakati za asubuhi ya jana.
Wazazi wa marehemu ambao wanaishi jijini Dar es salaam tayari wamewasili mchana huu kwa ndege na kwa mujibu wa redio moja inayorusha matangazo ya masafa ya fm hapa wazazi hao wameeleza kuwa binti yao alikuwa na matatizo ya homa ya kifafa ambacho inasadikiwa huenda ikawa chanzo cha kifo hicho ingawa uchunguzi unaendelea. Dereva taxi Bakari bado anashikiliwa na Polisi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni