Jumamosi, 6 Agosti 2011

AL SHABAAB WAUHAMA MJI WA MOGADISHU.

Kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al Shabaab, kinasema kuwa kimeondoka katika vituo vyake kadha ndani ya mji mkuu, Mogadishu.
Mogadishu, Somalia


Wakaazi wameiambia BBC kwamba waliona misafara ya wapiganaji ikiondoka katika mji huo.
Kuhama huko kunafuatia mapigano makali jana usiku.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachoisaidia serikali ya Somalia kimekuwa kikipigana na al Shabaab mjini Mogadishu katika siku za karibuni; ili kuweza kufikisha msaada wa chakula kwa wale walioathirika na ukame nchini Somalia.
Haijulikani kama wapiganaji hao wameondoka kabisa.
Msemaji wa serikali alielezea huo kuwa "ushindi wa dhahabu" kwa watu wa Somalia.
Lakini al Shabaab, ambayo inadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa nchi, ilisema wameondoka kufwatana na mikakati yao na iliahidi kufanya shambulio la kulipiza.
Baadhi ya wadadisi wanafikiri al Shabaab imepungukiwa na fedha kwa sababu wafadhili wao wa Arabuni wamewapunguzia msaada tangu al Shabaab kudhoofika kijeshi.
Wadadisi wanasema al Shabaab imewahi kuwahamisha wapiganaji wake mjini Mogadishu siku za nyuma, lakini safari hii inaonesha kuondoka kwao ni ushindi mkubwa kwa serikali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni