Jumamosi, 20 Agosti 2011

WIZI WA MAZAO KWA KUTUMIA MIZANI NA MAWE BANDIA WASHAMIRI VIJIJI VYA NACHINGWEA.

Ununuzi wa mbaazi  unaendelea lakini kukiwa na tatizo la mizani kupima uzito pungufu kwa vituo vingi vya kununua mazao, kinachofanyika ni kutumia mawe ya mizani yanayoiba uzito yaani kuonesha uzito pungufu ingawa mzigo uliowekwa kwenye mizani una kilo zaidi.Kijana huyu alikutwa na wakaguzi wa Halmashauri akinunua mazao akiwa na mawe sita lakini mawili kati yake yanatumika kuiba uzito.
Kati ya mawe haya sita, mawili ya katikati yanaiba uzito kati ya kilo 3 hadi 4 kwa kila kilo 20 zinazopimwa.
Mzani unaotumika, wahusika wamekamatwa na hatua za kisheria zinaendelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni