Jumatano, 10 Agosti 2011

WAKILI MAARUFU ARUSHA ASOMEWA MASHTAKA YA KUTAKATISHA FEDHA-MONEY LAUNDERING.

 Wakili Maarufu jijini Arusha Medium Mwalle amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashitaka 13 yanayodaiwa kumkabili likiwamo la kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye kaunti zake zisizo na maelezo sahihi (Money Laundering).
Wakili Median Mwalle wa nne toka kushoto mwenye suti nyeupe akiwa na Askofu Simon Makundi wa kanisa la Anglikan Arusha wa kwanza kushoto na Wakili Ezra Mwaluko wa pili toka kushoto wakati wa misa ya mapatano ya mgogoro wa kanisa mwaka jana, Mwalle alimwakilisha Askofu na Mwaluko aliwawakilisha waumini mahakamani.


Mwale alisomewa mashitaka hayo 13 jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha, Charles Magessa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali aliyejulikana kwa jina moja la Mallya.

Mara baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo Hakimu Magessa alitupilia mbali hoja za upande wa Mashitaka akidai maelezo katika hati hiyo hayakueleza wazi. Akisoma uamuzi mdogo baada ya kuahirisha kwa muda kesi hiyo, Magessa alidai, hundi zinazodaiwa kutumika kutoa na kuingiza fedha kwenye akaunti za mtuhumiwa hazikuelezwa zimetoka wapi na kwa nani, “Hati ya Mashitaka inatakiwa ieleze au itoe maelezo mafupi kulingana na mashitaka na vipengele husika. Kama haitafanyika hivyo ni wazi mwisho wa siku nguvu ya Mahakama hupotea bure,” alidai Magessa na kuongeza, “Lakini sheria inasema lazima hati ya mashitaka iwataje au imtaje mtu ili ajulikane ni nani. Hatua hii inasaidia mlalamikaji kujua nani anayemlalamikia.”

Alidai kutokana na hatua hiyo Hakimu Magessa alidai, kwamba Mahakama yake haitayapokea mashitaka hayo kuanzia la tatu hadi la 11 kutokana na makosa yalijitokeza, “Mashitaka haya kuwa ni makubwa, hivyo napendekeza yarudishwe yaandaliwe upya ili kusiwapo na mashaka kwenye hatui mpya itakayoletwa siku yoyote skutoka upande wa Serikali. “Sasa basi haitakuwa busara kuendelea na mashitaka ya haya hivyo naamuru mashitaka ya kwanza hadi la pili nayo yarudishwe yaje pamoja. Mtuhumiwa arudishwe mikononi mwa polisi kwani wao ndio wanataratibu za kumshikilia,” alidai Magessa.

Mwalle moja ya Mawakili waliojijengea umaarufu mkubwa anadaiwa kukamatwa Agosti 2, 2011 na polisi wa kimataifa wa Interpol, ambapo hadi jana tayari alikuwa amefikisha wiki moja akiwa anashikiliwa na polisi.

Aidha, hati ya mashitaka haikuweza kupatika kwa ajili ya kuandika kwa usahihi mashitaka hayo 13 kutokana na madai kwamba kulihitajika marekebisho.

Nje ya Mahakama

Hali ya hewa ilionekana kuwa nzito zaidi kwa baadhi ya mawakili waliokuwa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kujua hatima ya wakili mwenzao. Baada ya kutoka nje ya jengo la mahakama, wakili huyo alishindwa kuficha sura yake baada ya kukutana na kamera ya televisheni moja hapa nchini. Hatua hiyo ilimfanya Mwalle kuomba mpiga picha asiendelee kupiga picha kwa madai kuwa "atamharibia". Alilazimika kusimama kwa kuipa mgongo camera huku akiwa amezungukwa na maofisa wa polisi na usalama wa Taifa. Mara baada ya kuona wanacheleweshwa maofisa hao walimwamuru kuanza kutembea licha ya kamera hiyo kummulika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni