Alhamisi, 2 Juni 2011

SYRIA KUMECHAFUKA BAADA YA MTOTO KUUWAWA KWENYE MAANDAMANO.

Mtoto wa Miaka 13 Akatwa Uume na Polisi, Avunjwa Shingo, Miguu


Maiti ya Hamza
Mtoto wa kiume wa miaka 13, alikamatwa na kuteswa na polisi, alipigwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake, alikatwa uume wake, alivunjwa shingo na miguu yake, kosa alilolifanya ni kushiriki maandamano ya kuipinga serikali.
VIDEO utakayoiona chini, inamuonyesha mtoto Hamza Ali al-Khateeb mwenye umri wa miaka 13 wa kijiji cha Jiza, Dar'a nchini Syria ambaye video ya maiti yake imekuwa gumzo duniani baada ya baba yake kuiweka kwenye YouTube kuonyesha ukatili wa polisi wa Syria katika kuzuia maandamano ya watu wanaoipinga serikali ya rais Bashar al-Assad.

Mtoto Hamza alikamatwa na polisi aprili 29 wakati alipojiunga na wakazi wengine wa mji wake katika maandamano ya kuipinga serikali.

Mwili wake ulikabidhiwa baadae kwa wazazi wake ukiwa katika hali ambayo iliwafanya watu wengi wasiamini unyama wa polisi kwa mtoto mwenye umri mdogo kama Hamza.

Hamza alivunjwa shingo yake, miguu yake, alipigwa risasi kifuani na sehemu nyingine za mwili wake, na kama haitoshi polisi waliukata uume wake.

Wazazi wake walikabidhiwa mwili wake wauzike huku wakitishiwa wasiseme chochote au la watakiona cha moto.

Baba mzazi kutokana na uchungu wa unyama aliofanyiwa mwanae, aliamua kuchukua video ya maiti ya Hamza akionyesha wazi majeraha na unyama aliofanyiwa mwanae. Aliiweka Video hiyo kwenye YouTube.

Haukupita muda mrefu, baba yake Hamza alitiwa mbaroni na polisi na tangu wakati huo haijajulikana kama yuko hai au la huko alipo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni