Alhamisi, 9 Juni 2011

BIG BROTHER NA MAADILI YA KITANZANIA,BHOKE ALIWA URODA LIVE.

Bhoke na Ernest

Safari ya Tanzania kwenye Big Brother Africa imemalizika kwa mwanadada Bhoke kutupwa nje ya mashindano hayo baada ya kutajwa mara nyingi na wenzake.

Achana na kutoka kwa Bhoke, kilichobaki sasa kwenye historia ni video ya Bhoke akiliwa uroda Live kwenye luninga na Ernest wa Uganda. Video hiyo imezagaa kwenye YouTube na mitandao mingi barani Afrika.

Ingawa kipindi hicho huangaliwa na watu wengi wa rika mbalimbali, kitendo cha Bhoke kufanya mapenzi mbele ya kamera kimenifanya nijiulize nini tunajifunza toka kwenye Big Brother Africa.

Ingawa hatujui kama mapenzi yao yalikuwa ya kweli au na kama mapenzi hayo yataendelea nje baada ya wote wawili kutolewa kwa pamoja juzi, lakini imeonyesha ni jinsi gani jinsi maadili yetu ya kiafrika yalivyogeuzwa na maendeleo ya teknoojia na kuwa kama ya watu wa mataifa ya magharibi.

Ingawa inasemekana kuwa washiriki wa Big Brother walipimwa HIV na magonjwa mengine ya zinaa kabla ya kuruhusiwa kushiriki mashindano hayo, bado mashindano haya sidhani kama yanawafundisha watu maadili mema ya kuepukana na ngono zembe

Maoni 3 :

  1. wamejizalilisha

    JibuFuta
  2. Bhoke kumpenda ernest si tatizo lakini kinachosikitisha ni kuliwa uroda hadharani tena wakati dunia nzima inaona wakiwemo wazazi wake ndugu zake na pengine mtoto wake kama anae, amejitetea kuwa akirudi tena atafanya hivyo hivyo then naogopa kuwa huenda siku moja ndani ya kipindi chake cha TV anaweza , manake kama ni pepo basi analo kutoka chini ya bahari loooh,

    JibuFuta
  3. hata makahaba wa ambiance na jollys hawafanyagi mapenzi hadharani

    JibuFuta