Ijumaa, 3 Juni 2011

MBOWE ANATAFUTWA NA MAHAKAMA.

Friday, June 03, 2011 11:16 AMMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imeliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bw. Freeman Mbowe kwa kosa la kutofika mahakamani kutokana na kesi inayomkabili.
Hakimu Magesa alitoa hukumu hiyo baada ya mshitakiwa huyo kutofika mahakamani kujisalimisha katika kesi inayowakabili na viongozi wenzake wa juu wa chama hicho kwa kosa la kufanya mkusanyiko Januari 5 mwaka huu isivyo halali.

Wengine wanaojumlishwa katika kesi hiyo akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, Bw. Phillemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini na Bw. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini ambapo wao walijisalimisha

Washtakiwa wengine ni mchumba wa Dk. Slaa, Bi. Josephine
Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba.

Hakimu Magesa alitoa hukumu hiyo kwa mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani na matokeo yake hakufanya hivyo wala mdhamini wake naye hakufika.

“Hivyo kutokana na kitendo hicho ni kosa kisheria, Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa hata kama alikuwa na udhuru”alisema Hakimu Magesa

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 24, mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni