Jumamosi, 12 Novemba 2011

STARS YAIFUNGA CHAD 2-1

Kocha wa Taifa Stars Jan Poulsen


Na Edo Kumwembe, N'djamena, Chad
FALSAFA ya kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Jan Poulsen ya kushambulia mwanzo mwisho katika mechi dhidi ya Chad, ilizaa matunda jana baada ya kuibuka na ushindi wa kwanza ugenini wa mabao 2-1 mechi ya kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi fainali za Kombe la Dunia, shukrani kwa Nurdin Bakari aliyefunga bao la ushindi kwenye mechi hiyo.

Nurdin aliyeingia toka benchi, alifunga bao hilo katika dakika ya 85 akimaliza pasi nzuri ya Thomas Ulimwengu na kuwanyamazisha mashabiki wa Chad waliojazana kwenye Uwanja wa Idriss Mahamat.Huu ni ushindi wa kwanza ugenini wa kocha Poulsen tangu aanze kuifundisha Stars akichukua nafasi ya kocha Marcio Maximo.
Matokeo haya ni mazuri kwa Stars na angalau yametuliza kiu ya mashabiki wa soka nchini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wanyonge kila timu yao inapocheza.Ili iweze kuingia hatua ya makundi, sambamba na Morocco, Ivory Coast na Gambia, Stars itahitaji sare tu katika mechi ya marudiano itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wiki ijayo.
Mara baada ya mchezo kumalizika, Poulsen alisema kikosi chake kilicheza vizuri, na anashukuru mfumo wake wa kushambulia mfululizo ulizaa matunda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni