Jumapili, 6 Novemba 2011

MGOMO WA KUUZA MAFUTA YA PETROL MIKOA YA KUSINI JANA NA LEO.

Kumekuwa na mgomo wa kimyakimya wa kuuza nishati aina ya Petrol kuanzia jana hadi leo katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kisingizio kuwa mafuta yameisha au pampu mbovu. Uchunguzi uliofanywa na blogu hii umegundua kuwa  sababu ni mgomo maalumu baada ya EWURA kupunguza bei ya nishati hiyo, Maeneo ya Rwangwa, Lindi, Ndanda, Masasi, Nachingwea na Nanyumbu nishati hiyo haikupatikana jana na kusababisha watu kununua mtaani(videbe) kwa bei kati ya shilingi 3500 hadi 4500 kwa lita jana na leo, uuzaji wa dizeli na mafuta ya taa unaendelea, EWURA mjue hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni