Jumanne, 1 Novemba 2011

PICHA YA LEO; SHOKA LANASA KICHWANI BAADA YA KUPIGWA NA MAJAMBAZI

Juzi saa 12 asubuhi hospitali ya taifa Muhimbili imempokea mgonjwa anayeitwa Mussa Shabani(42) akiwa na shoka iliyonasa kichwani kwake kama picha inavyooneka.
  
Imeelezwa kuwa Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata, Majambazi yalipofika nyumbani kwa 
Mwakyusa yalimjeruhi kwa shoka mlinzi huyo yalifungua spea za gari aina ya Toyota verosa. 
Kwa bahati nzuri Mwakyusa alishtuka na ndipo majambazi hayo yalipokimbia na kutoweka yakimuacha mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.
 
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa mahututi.
Jumaa Almasi ambaye ni afisa uhusiano mkuu wa MOI  amethibitisha tukio hilo na kusema  ''Ni kweli Mussa amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa hivi yupo chumba cha wagonjwa mahututi''
Chanzo; http://www.kalulunga.blogspot.com/

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni