Alhamisi, 3 Novemba 2011

ALIYEKUTWA NA FUVU LA BINADAMU AFUNGWA MIAKA 10 JELA.

Picture
Fatma Kachingo (aliyeshikilia fuvu) akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi mkoani Morogogo
Fatuma Kachingo (42) ambaye anadaiwa kuwa ni mganga wa jadi katika kijiji cha Wami Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, anayedaiwa kukutwa na fuvu pamoja na ngozi ya binadamu, amehukumiwa kwenda jela miaka 10 kufuatia kukiri kosa la kukutwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria.


Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Morogoro, Nuru Prudencia Nasari baada ya mshitakiwa namba moja ambaye ni mwanamke kukiri shitaka lake huku mumewe akirudishwa mahabusu baada ya kukana shitaka wakati walipofikishwa katika mahakama hiyo kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka hilo wote pamoja.


Hakimu Nasari akisoma hukumi hiyo kwa Fatuma Kichango alisema kuwa kosa alilokutwa nalo mtuhumu la kumiliki viungo vya binadamu ni kinyume cha sheria za nchi hivyo anatoa hukumu ya kwenda jela miaka 10 ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo ambapo miaka hiyo inatokana na utetezi wa mshitakiwa kwa kuwa hajawahi kushitakiwa na kosa lolote la jinai na kwamba ana mtoto mdogo anayemtegemea kwani jambo hilo ni la kutisha katika jamii.


Nasari alisema pia mahakama imeona kuwa ni kuwa na vitu kama hivyo na kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanamiliki vitu kama hivyo.


Awali akisoma shitaka, Mwendesha Mashitaka wa polisi Lameck Wabi alidai kuwa washitakiwa hao kwa pamoja walikutwa na Fuvu na ngozi ya binadamu pamoja na vifaa vingine vinavyodhaniwa kuwa vya kishirikiana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni