Jumatatu, 21 Novemba 2011

MBUNGE JOSEPH MBILINYI AZINDUA KITABU CHA HISTORIA YA MAISHA YAKE-SUGU.

Mbunge Joseph Mbilinyi akiwa na kitabu chake kiitwacho SUGU.
Mh. Joseph Mbilinyi.


Kuna video moja youtube ambayo inamwonesha Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilini almaaruf "Sugu" akiwa na kitabu ambacho anapasha kuwa kinayazungumzia maisha yake (biography) tangu angali mtoto mdogo, harakati zake katika muziki na hatimaye kugombea uwakilishi wa wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hajatamka kitabu kitapatikana madukani lini, kitapatikana katika maduka na wakala gani, wasambazaji ni akina nani, wala mawasiliano ya jinsi ya kukipata.


Nadhani ni hatua mojawapo nzuri na changamoto kwetu Watanzania wote kuwa na tabia ya kupenda kuandika na kujisomea vitabu mbalimbali.


Sina shaka kuwa kitabu kama cha "Sugu" kitakuwa chachu kwa watu wa rika mbalimbali, hasa vijana, ambao wangependa kujifunza mema ya kuigwa katika mapito ya Mheshimiwa Mbilinyi

source: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz1eHmldeZw

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni