Ijumaa, 18 Novemba 2011

AJARIBU KUMUUA OBAMA KWA VILE ANAUCHUKIA UKRISTO.



NewsImages/6070310.jpg
Oscar Ortega-Hernandez
Kijana mwenye umri wa miaka 21 amefikishwa mahakamani kwa kosa la kujaribu kumuua Obama akidai Obama anapinga ukiristo. Kijana huyo alipiga risasi mbili kwenye Ikulu ya Marekani ambazo zilivunja vioo vya mojawapo ya madirisha ya Ikulu.
Kijana Oscar Ortega-Hernandez akitumia bunduki za masafa marefu alijaribu kumuua rais wa Marekani, Barack Obama akisema kuwa Obama anauchukia ukristo.

Oscar alipandishwa mahakamani mjini Pittsburgh akituhumiwa kumuua Obama kwa jaribio lake alilolifanya wiki iliyopita.

Obama, mkewe na watoto wao hawakuwepo ikulu wakati Oscar alipopiga risasi mbili toka kwenye makutano ya barabara mbele ya viwanja vya ikulu umbali wa mita 750 toka kwenye jengo la ikulu.

Maafisa wa Ikulu walisema kuwa risasi moja ilivunja kioo cha mbele cha Ikulu lakini ilizuiliwa na kioo cha pili ambacho hakipitishi risasi.

Risasi ya pili iligonga maeneo ya nje ya Ikulu.

Magari mawili yalionekana yakitoweka kwa kasi toka kwenye eneo la tukio.Gari moja lilikutwa likiwa limetelekezwa sehemu likiwa na bunduki ya masafa marefu.

"Ortega-Hernandez amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kumuua Rais Obama", alisema mwanasheria msaidizi wa Marekani, James Kitchen.

Oscar alihamishwa rumande mjini Washington akisubiri kupandishwa tena kizimbani. Akipatikana na hatia atatupwa rumande maisha

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni