Jumamosi, 12 Novemba 2011

POLISI WALIOCHUKUA RUSHWA KWA MFUGAJI SINGIDA WAFUKUZWA KAZI.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Selina Kaluba.
JESHI la Polisi Mkoani Singida limewafukuza kazi askari wake wawili waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kijeshi, na hivyo kuthibitika ni kweli walichukua rushwa ya Sh milioni tisa kutoka kwa mfugaji mmoja wa ng’ombe.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Ayoub Tenge, iliwataja askari hao kuwa ni E.931 koplo mpelelezi Lukololo na E. 3106 Konstebo Joseph Pazza.

Tenge alisema, akari hao baada ya kutiwa hatiani katika Mahakama ya Kijeshi kwa makosa yaliyokuwa yanawakabili, wamefukuzwa kazi.

Alisema, Lukololo na Pazza tayari wamefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Singida na kuunganishwa na washitakiwa wengine watatu.

Washitakiwa hao wanatakiwa kujibu mashitaka yanayowakabili ambayo waliyotenda kwa pamoja mapema Oktoba 2, mwaka huu huko katika kijiji cha Iyumbu Singida Vijijini.

Aliwataja washitakiwa wengine kuwa ni Leonard Kahema, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkongwa, Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, Sung’wa Nkuba pamoja na Hussein Juma wote wakazi wa kijiji cha Iyumbu mkoani Singida.

Alisema, washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa la kujipatia kiasi cha Sh milioni tisa kutoka kwa mfugaji wa ng’ombe aitwaye Shigela Nkonga, mkazi wa kijiji cha Nkongwa Wilaya ya Uyui baada ya kumbambikizia kesi ya kuwa na viungo vya binadamu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni