Jumatano, 9 Novemba 2011

MBUNGE AHOJI UHALALI WA UBAGUZI SHULE ZA AL-MUNTAIIR

SHULE zinazomilikiwa na madhehebu ya Isnaasheri za Al Muntazir zimelalamikiwa kufanya ubaguzi wakati wa udahili wa wanafunzi.

Malalamiko hayo yametolewa na Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kassim (CUF) wakati akiuliza swali la nyongeza kama serikali inafahamu ubaguzi huo.

“Je, Serikali inafahamu kama shule za kidini za al Muntazir zina ubaguzi wa madhehebu ambapo kigezo cha kwanza kupata lazima uwe Shia?” alihoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema serikali inahitaji majina ya shule hizo ili iweze kufanyia kazi.

Kwa upande wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa akizungumzia motisha kwa walimu wanaopangiwa maeneo ya pembezoni, alisema serikali imeanza kutoa Sh 500,000 kama fedha za kujikimu kwa walimu hao.

Alisema lengo la kutoa fedha hizo kwa walimu wanapokwenda maeneo yenye changamoto ni kuwafanya wavutiwe kusomesha katika maeneo hayo.

Waziri Kawambwa alitoa ufafanuzi huo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali(CCM) aliyetaka kufahamu kama serikali imeweka motisha kwa walimu wanaopangiwa katika maeneo yenye changamoto.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema) aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kuondoa tofauti za kielimu kati ya wenye nacho na wasio na uwezo, kijinsia na baina ya maeneo yaliyoendelea, Mulugo alisema serikali inatoa elimu kwa usawa.


Maoni 1 :

  1. Discrimination in its own right is not bad at all. It all depends on whether the discrimination is fair or unfair.

    Nami naamini kama watoto watakataliwa eti kwasababu shule inaendesha dhehebu lake, haitakuwa sawa hivyo...labda iwe sawa kama watoto hao wasio wenye dini ya shule, baada ya kuingia shuleni mule, INAJULIKANA KABISA KWAMBA WATAKUJA KUKATAA KUJIJUMUISHA NA DESTURI YA SHULE HIYO KI-DINI!

    JibuFuta