Jumamosi, 17 Septemba 2011

RAIS KIKWETE AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA MIKOA IKULU LEO ASUBUHI


 Rais Dkt. Jakaya Kikwete , akimwapisha Mwantum Bakari Mahiza, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo asubuhi katika Viwanja vya Ikulu Dar. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo.



Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiteta jambo baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa Ikulu,jijini Dar es Salaam leo.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni.Sherehe za kuwaapisha wakuu hao wapya wa mikoa imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.Pichani ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Tabora. Bi.Fatuma Mwassa akila kiapo mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na kukabidhiwa miongozo ya kazi. 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Leonidas Tutubert Gama, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Fabian Inyasi Massawe, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa walioteuliwa kushika nyadhfa hizo baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo, asubuhi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni