Jumapili, 18 Septemba 2011

KONDOMU ZA KIKE ZA CHINA NI NDOGO KWA WAAFRIKA KUSINI

'Kondomu za Wanawake Toka China ni Ndogo Sana'

NewsImages/5952702.jpg
Mahakama nchini Afrika Kusini imezuia uamuzi wa serikali kununua kondomu za wanawake toka China kwa kuwa kondomu hizo ni ndogo na haziwafiti vizuri wanawake wa nchini Afrika Kusini.
Mahakama ya nchini Afrika Kusini imeizuia serikali ya Afrika Kusini Kuendelea na mpango wake wa kununua kondomu za wanawake milioni 11 toka nchini China kwa kuwa kondomu hizo ni ndogo sana kwa wanawake wa Afrika Kusini.

Wizara ya fedha ya Afrika Kusini iliingia mkataba na kampuni ya Siqamba Medical, kununua kondomu za wanawake zinazoitwa Phoenurse toka China, gazeti la Beeld liliripoti.

Kampuni nyingine inayoitwa Sekunjalo Investments Corporation, ambayo ilinyimwa mkataba huo na serikali iliamua kwenda mahakamani mjini Pretoria kupinga rufaa uamuzi huo wa serikali ikisema kuwa kampuni hiyo ya nchini Afrika Kusini inatengeneza kondomu zenye ukubwa wa asilimia 20 zaidi ya kondomu zinazotengenezwa nchini China.

Jaji wa mahakama hiyo ya Pretoria alitoa uamuzi wa kuuzuia uamuzi wa serikali akisema kuwa kondomu toka China ni ndogo sana kwa wanawake wa Afrika Kusini na pia zimetengenezwa kwa vifaa ambavyo havijathibitishwa na shirika la afya la dunia (WHO).

Afrika Kusini inaongoza duniani kwa idadi kubwa ya watu walioathirika na HIV duniani.

Jumla ya watu milioni 5.38 kati ya milioni 50 waliopo nchini Afrika Kusini ni waathirika wa HIV

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni