Jumamosi, 17 Septemba 2011

BAKARI MSULWA AMKUMBUKA MAREHEMU ABISAY STEVEN

Mtangazaji Radio Japan, Bakari Msulwa.

 
Hiki ni kionjo katika makala ya kumbukumbu ya mtangazaji mahiri, Bakari Msulwa wa RTD ambaye sasa yupo Redio Japani NHK, akimkumbuka mfanyakazi mwenzie wa RTD, aaliyeaga dunia wiki jana, Abisay Stephen.
---

Lakini sababu ya tatu, kati ya mwaka 2000 na 2008 nilikuwa nje ya jiji la Dar es salaam, niliondoka hapo kwa tiketi ya RTD. Mambo mengi yakabadilika , RTD ikawa TUT na baadaye TBC, miye nikiwa nawajibika mikoani.

Niliendeleza utumishi wangu katika mikoa ya Mwanza, Arusha , huko Zanzibar (Unguja na Pemba) na baadaye Shinyanga. Na nilipohamishiwa tena Dar es salaam mwezi Mei mwaka 2008 nilikutana tena na Marehemu Abisay Stephen , tukafanya kazi kwa mwezi mmoja katika ofisi moja ya ‘taifa’kabla sijakuja hapa Tokyo , Japani kujiunga na Idhaa hii ya Kiswahili ya Redio Japani-NHK. Nahisi kipindi cha miaka tisa cha kuwa mbali na Abisay na watangazaji wenzangu wa makao makuu , mengi yamebadilika.

Tabia za watu , mienendo, mtazamo na hata harakati zao. Nimekuwa wa mikoani na wao wa makao makuu. Na huu ndio ukweli. Na sasa kuna channeli zaidi ya nne, TBC 1, TBC Taifa, TBC FM na TBC International…mabadiliko makubwa. Vijana wengi, wasomi wengi na vipaji vingi sasa kuliko pengine enzi hizo. Nilichelea, kama naweza kuwa na ujasiri wa kuandika. Lakini bado naaamini kuwa sitakuwa nje sana ya mstari, na kama itakuwa hivyo nastahili kusamehewa.

Nimemuona hayati Abisay Stephen mwaka 1989, nilipojiunga RTD . Rasmi nilianza kazi mwaka 1990, wakati huo ndani ya majengo ya RTD kulikuwa na mtindo wa uhamisho wa ndani wa kiidara ambapo watangazaji walikuwa wakihamisha kila viongozi wanapoona inafaa. Ilitokea tu, nilifanya kazi na Marehemu Abisay, katika Iliyokuwa Idhaa ya nje ya RTD, ‘External Service, Idhaa ya Taifa na baadaye Idhaa ya biashara. Kwa kawaida kila asubuhi mara baada ya kikao cha viongozi wa idara maarufu kama ‘Post Mortem’ , Idara na Idhaa zetu nazo zilikutana miongoni mwa watendajji wake . Hao ndipo nasi tulipata kusikia ‘maamuzi na maelekezo kutoka juu’ na wakati huu tukielezwa na Abisay.

Hayati Abisay , aliweza kueleza msimamo huo kwa lugha isiyokwaza , akidondoa moja baada ya jingine na kuhimiza utekelezaji. Alikuwa rafiki na bosi wa kila aliye chini yake. Alikuwa tayari kusikia changamoto za ‘vijana ‘ na mara zote aliishia kutupa moyo kuwa kwa kufanya hivyo tutafika tunakokenda. Ndipo nilipogundua uwezo wake mkubwa wa kupambanua mambo, kufuatilia masuala ya kihabari na kujenga mtandao utakaowezesha kufanikisha azima iliyopo. Mara kadhaa aliwahi kunipa majukumu na kunipa moyo kuyatekeleza. Hakuwa mtu aliyeogopa mabadiliko ya kimaendeleo na aliwahi kudokeza kuwa kuna wakati alioonekana kukengeuka alipopishana na ‘wenzake‘ katika mambo Fulani na na kuwajiwajibishwa kwa ukengeukaji huo, kimya kimya’.

Nakumbuka aliwahi kusema kuwa ‘tunahitaji kufanya kazi kwanza , kabla ya kulalamika kwa masuala binafsi’


source: wavuti.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni