Ijumaa, 30 Septemba 2011

NYUMBA ZABOMOLEWA KUNDUCHI MTONGANI JANA.

Nyumba Kunduchi Zabomolewa


Thursday, September 29, 2011 10:41 AMJESHI la Polisi limebomoa nyumba za wakazi eneo la Kunduchi Mtongani kwa kile kilichodaiwa kuwa zimejengwa ndani ya eneo la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).


">Majira ya alfajiri jana ubomoaji huo ulianza na nyumba ambazo idadi yake haijafahamika kamili lakini zilizomolewa katika taarifa ya awali zimedaiwa ni zaidi ya 30
Ubomoaji huo uliendelea kwa kusimamiwa na Kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwa na mabomu ya machozi, silaha za moto na magari ya maji ya kuwasha.

Sababu za awali zinadai nyumba hizo zimezidi mita 50 kuingia sehemu zinapohifadhiwa silaha za jeshi kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni