Jumanne, 6 Septemba 2011

KATIBU MKUU WIZARA YAARDHI NA WAKURUGENZI WAWILI JELA MIEZI SITA AU FAINI KWA KUIDHARAU MAHAKAMA.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.

Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi Ndg. Patrick Rutabanzibwa jana alihukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki tano hadi kufikia alhamis juma hili, akitoa hukumu hiyo Jaji Nchimbi wa Mahakama ya Ardhi alisema Katibu Mkuu na Wakurugenzi Sichone na Bi. Bura pia wanahusika na adhabu kama hiyo kwa kukaidi amri ya mahakama inayowataka kusaini hati za matoleo ya viwanja viwili vyenye mgogoro ambao umeisha kwa makubaliano ya wabishani huko Msasani Peninsula.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni