Jumanne, 27 Septemba 2011

MTOTO MWENYE SURA MBLI AZALIWA PAKISTAN, MUNGU MKUBWA.


NewsImages/5968126.jpg
Mtoto mwenye sura mbili aliyezaliwa nchini Pakistan
Mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kwenye wadi ya wazazi ya hospitali moja nchini Pakistan ili kumshuhudia mtoto mwenye kichwa chenye sura mbili aliyezaliwa juzi nchini humo.
Mtoto huyo alizaliwa usiku wa kuamkia ijumaa akiwa na kichwa kimoja chenye sura mbili tofauti.

Mtoto huyo aliyezaliwa kwa njia ya kawaida bila ya operesheni alikuwa na uzito wa kilo 3.2. Alizaliwa kwenye mji wa Palandri uliopo Azad Kashmir nchini Pakistan.

Hali aliyo nayo mtoto huyo inajulikana kitaalamu kama "Craniofacial duplication" ambapo kichwa chake kilikuwa na sura mbili ambapo alikuwa na midomo miwili, macho manne, pua mbili isipokuwa tu alikuwa na masikio mawili tu.

Ana ubongo mmoja na kwajinsi maumbile yake yalivyoungana madaktari wanasema kuwa ni vigumu sana kumfanyia operesheni ya kurekebisha sura yake ili awe sawa na watoto wengine.

Daktari wa hospitali ya HFH aliyozaliwa mtoto huyo aliyejitambulisha kama daktari Nasira, alisema kuwa wana matumaini madogo sana mtoto huyo ataishi muda mrefu kwani hadi sasa anashindwa kupumua vizuri na analishwa kwa kutumia mrija.

"Tuna matumaini madogo ya kunusuru maisha ya mtoto huyu", alisema daktari Nasira.

Mtoto huyo alizaliwa katika familia ya bwana Khalil Ahmed na mkewe Shahida Perveen ambao wana watoto watatu waliozaliwa bila ya kuwa na dosari yoyote kwenye maumbile yao.

Mama wa mtoto huyo bado amelazwa hospitali pamoja na mtoto wake ambaye amelazwa kwenye kitengo maalumu akipatiwa matibabu maalumu ya kunusuru maisha yake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni